Mabingwa watetezi Yanga wamekamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kuizaba timu ya Tanzania Prison kwa Jumla ya magoli 4-2 katika mchezo uliyopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
mashujaa wa Yanga katika mchezo huo alikuwa ni Mrisho Khalfani Ngasa aliyefunga magoli mawili, Kigi Makasi na Athumani Iddi Chuji kwa shuti la mbali.
Magoli ya Tanzania Prison yalifungwa na John Matei na Jackob Ibrahim.
Yanga imemaliza msunguko wa kwanza wa Vodacom Premiur League ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 21 ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC inayoshikilia nafasi ya pili huku wakiwa pointi 12 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Simba wenye pointi 33.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment