Klabu ya timu ya Yanga imeitaka mikoa yote ya Tanzania bara kuanza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi katika matawi yake kwa kufuata katiba ya mwaka 2008 ambayo kwa sasa imefanyiwa marekebisho.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Jengo jipya la Timu hiyo yenye maskani yake Jangwani Afisa Habari wa Yanga Luis Sendeu amesema lengo la kufanya hivyo ni kutokana na kuimarisha matawi ambapo kwa kipindi kirefu nafasi nyingi zilikuwa zikikaimiwa.
Sendeu ameongeza kuwa Mchezaji wao Obren Circovic ameondoka jana jioni kuelekea Nchini kwao Serbia kwa ajili ya Kuoa ambapo atakaa kwa wiki mbili.
Lakini pia amesema Mchezaji Nadir Haruob Canavaro ambae amerudi kutoka Cannada baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi mitatu kuwa ni mchezaji wao halali mpaka sasa na endapo timu yoyote itamuhitaji basi milango ipo wazi kuzungumza nao kwani bado anamkataba wa miaka miwili.
Akizungumzia kuhusu maendeleo ya timu yake Sendeu amesema Klabu Yanga baada ya kumaliza mchezo wake dhidi ya Tanzania Prison itakuwa mapumzikoni kwa muda wa wiki moja kabla ya kuingia kambini ili kujindaa na Mashindano ya Klabu Bingwa yatakayoaanza Mwezi Januari hapo mwakani.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment