Akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF Maximo amesema kuwa kutofanya vizuri kwa Taifa Stars hata yeye hapendi matokeo mabaya lakini tukumbuke tulipotoka na sasa tupowapi na kufanya vizuri kwa timu si mafanikio ya muda mfupi jinsi Watanzania tunavyofikiri.
Maximo ameongeza kuwa tusifikirie wachezaji wa Timu ya Taifa tulionao kwa sasa ambao umri wao unafikia ukingoni bali tuwe na mipango endelevu ikiwa ni pamoja na kuimarisha michezo kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 na 21 ili kupata Timu ya Taifa Bora hapo baadae.
Timu ya Taifa inatarajiwa kuingia kambini kesho kutwa kujiandaa na Mashindano ya Chalenji itakayoshirikisha jumla ya Nchni 11 itakayoanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu huko Nchni Kenya.
No comments :
Post a Comment