Kombe la Dunia lipo ziarani nchini Tanzania. Ziara hiyo imezinduliwa rasmi leo jioni nchini Tanzania na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Ziara ya kombe hilo katika sehemu mbalimbali duniani, ni ishara ya kuwapa fursa mashabiki mbalimbali wa soka ulimwenguni,nafasi ya kuliona kombe hilo “live” na hata kupiga nalo picha kwa kumbukumbu nk. Hizo zote ni miongoni mwa shughuli mbalimbali kuelekea South Africa 2010.
Wakati nikimuangalia Rais Kikwete akiwa amejawa na tabasamu wakati akilinyanyua kombe hilo na kulibusu,nilijiuliza, hivi itakuja tokea kweli siku moja Rais wa Tanzania(yeyote yule atakayekuwa madarakani) kulinyanyua Kombe la Dunia baada ya kulipokea toka mikononi mwa nahodha wa Taifa Stars baada ya kulitwaa?
Well…naamini kila kitu kinawezekana. Sina tu uhakika kama tuna mipango madhubuti(ya mbali au karibu) ya kutimiza ndoto hizo.Tusiishie tu kuliona kombe kwa mbali au kulinyanyua pale tusipostahili.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amelinyanyua juu kombe la FIFA la dunia wakati alipozindua rasmi ziara ya kombe hilo hapa nchini na kupiga nalo picha jioni hii kwenye uwanja wa taifa rais aliingia kwenye kibada maalum kilichojengwa kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuhifadhia kombe hilo akalibeba na kulinyanyua juu huku akilibusu kombe hilo , Rais Jakaya amemtaka rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Rodger Tenga pamoja na kamati zake kufanya kazi ya kusimamia na kuinua kiwango na vipaji vya mpira wa miguu nchini badala ya kusimamia timu ya taifa tu na mapato ya milangoni kwani hawako TFF kwa ajili ya kujenga nyumba zao Binafsi bali wapo kwa ajili ya kuendeleza na kukuza soka nchini, Rais Jakaya amelaani kitendo cha shirikisho hilo kuwapa adhabu ya kuwafungia muda mrefu hadi miezi sita wachezaji na kusema hiyo ni kuwakomoa na kudidimiza vipaji vyao badala ya kuviendeleza ziara ya kombe la FIFA la dunia inaratibiwa na wadhamini wa kombe hilo Cocacola na linatembezwa nchi mbalimbali Duniani, aliyeko kulia katika picha ni Hedi Hamer mwakilishi wa FIFA.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
6 days ago
No comments :
Post a Comment