Mnyama Simba avunja rekodi ya klabu Yanga katika ligi kuu Tanzania kwa kumaliza duru la kwanza wakiwa na jumla ya 33 ikiwa ni pointi tatu zaidi Yanga katika msimu uliyopita.
Simba imevunja rekodi hiyo ya Yanga iliyowekwa msimu uliyopita baada ya kuwazamisha mabingwa Ngao ya Hisani Mtibwa Suger katika mchezo uliyopigwa kunako uwanja wa Uhuru.
Wauaji wa Simba ni Mussa Hassan Mgosi, Uhuru Suleiman na David Naftari aliyefunga goli la tatu akiunganisha mpira uliyopigwa na Emmanuel Okwi.
Simba imemaliza duru la kwanza la ligi kuu ikiwa inaongoza kwa jumla ya pointi 33 ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment