Mfanyakazi
katika Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura
(aliyevalia fulana ya Yanga kulia) akiwaonyesha kocha wa timu ya Yanga,
Thom Sainfiet, na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo jinsi bia
zinavyopikwa jana Alhamisi, wakati timu hiyo yenye maskani yake katika
mitaa ya Twiga/Jangwani jijini, ilipofanya ziara yake katika kiwanda
hicho kilichopo Ilala, jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto) akiwa na
beki mpya wa timu ya Yanga, Mbuyu Twite (katikati) na Msemaji wa timu
hiyo, Louis Sendeu jana Alhamisi wakati timu hiyo yenye maskani yake
makutano ya Mitaa ya Twiga/Jangwani jijini Dar es Salaam ilipofanya
ziara katika kiwanda hicho. Anayeonekana nyuma yao ni kocha wa timu
hiyo, Thom Sainfiet.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto kabisa)
akiwa na baadhi ya viongozi wa vitengo mbalimbali vya Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) pamoja na wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu
ya Yanga juzi Alhamisi wakati mabigwa hao wa Kombe la Kagame
walipotembelea kiwanda cha TBL kilichopi Ilala jijini Dar es Salaam.
Wachezaji
wa timu ya Yanga pamoja na Benchi la Ufundi la timu hiyo, pamoja na
baadhi ya viongozi wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi
wanawake wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) jana Alhamisi wakati timu
hiyo ilipofanya ziara kiwandani hapo, Ilala jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MABINGWA wa Kombe la Kagame Yanga, jana
wamefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia nchini (TBL),
kilichopo Ilala jijini Dae es Salaam, ambacho kinaidhanmini klabu hiyo
kupitia bia ya Kilmanjaro,.
Akiongea katika
ziara hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, alisema timu yake
iliamua kufanya ziara yao katika kiwanda hicho, ili kuweza kujionea
mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na kampuni hiyo inayozalisha vinwaji
mbali mbali, ikiwamo Kilimanjaro.
Alisema kuwa, Kilimanjaro Premium Lager
imekuwa ikiwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa mambo
mbalimbali ya kimichezo, ikiwa ni pamoja na kuwapatia magari ya usafiri
jezi pamoja na vifaa, na kwamba wamefurahishwa na aina ya mapokezi
waliyoyapata kiwandani hapo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa
kuthamini timu yao.
"Tunawaomba muendele na moyo huo huo kwani
sisi kama Yanga, tunaamini kuwa huwezi kutenganisha mafanikio ya klabu
yetu kwa sasa na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager, na kwamba kwa
pamoja, tutaweza kulifikisha soka la Tanzania katika kilele cha ubora,"
alisema Sendeu.
Awali, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George
Kavishe alisema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo cha Yanga kuamua
kuacha shughuli zao na kutembelea kiwanda chao, kujionea kazi za
uzalishaji zinavyofanywa kiwandani hapo.
Alisema kuwa Kilimanjaro Premium Lager
inathamini mchango wa timu ya Yanga katika maendeleo ya soka la Tanzania
na ndio maana imekuwa ikiidhamini timu hiyo, huku akibainisha kuwa
wataendela kuidhamini kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo.
Thamani ya udhamini wa Kilimanjaro kwa
Yanga unafikia jumla ya dola za Kimarekani 1.5milioni (Shillingi Bilioni
mbili za Kitanzania) kwa mwaka. Pesa hizi hutolewa kwa ajili ya
shughuli mbali mbali kama kusajili wachezaji wapya wa kimataifa, mabasi,
vifaa vya michezo na kukiwezesha Mkutano Mkuu wa Mwaka.
"Tunafanya hivi tukiwa na nia ya kupeleka
soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio… Ni dhahiri kuwa Yanga
imekuwa ikifanyia mambo makubwa kwani imekuwa ikiwapatia vijana
mbalimbali ajira kupitia timu yao.
"Ushirikiano wetu na Yanga unatokana na ukweli kwamba, ni kati ya timu zenye wapenzi wengi zaidi hapa nchini," alisema Kavishe
No comments :
Post a Comment