NEW YORK, Marekani
Wakati
Serena akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus
Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2
5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber
NYOTA
anayeshika nafasi ya nne katika viwango vya ubora wa tenisi duniani,
Serena Williams hakupata shida kufuzu raundi ya tatu ya micuano ya Wazi
ya Marekani ‘US Open’ baada ya kupata ushindi wa moja kwa moja dhidi ya
Mhispania Maria Jose Martinez Sanchez.
Bingwa
huyo wa michuano ya Wimbledon na Olimpiki, alitumia muda wa saa moja na
dakika 22 (1:22) kuibuka kidedea kwa seti mbili kwa bila za 6-2 6-4
dhidi ya nyota asiyekuwa na kiwango Sanchez.
Wakati
nyota huyo akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open,
Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha
6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber.
Nyota
namba mbili kwa ubora duniani, Agnieszka Radwanska alilazimika kufanya
kazi ya ziada kutoka nyuma na hatimaye kumshinda Mhispania Carla Suarez
Navarro kwa 4-6 6-3 6-0.
Kwa
upande wake mkali wa mchezo huo raia wa Serbia, Ana Ivanovic aliibuka
kidedea na kutinga raundi ya tatu ya michuano hiyo kwa ushindi wa 6-2
6-2 dhidi ya Msweden Sofia Arvidsson.
Katika
raundi ya tatu, Ivanovic anatarajia kupata upinmzani mkali kutoka kwa
yoso wa miaka 19 Sloane Stephens, yoso aliyeingia katika 50 bora ya
wacheza tenisi wanamama, aliyetinga hatua hiyo kwa kumchapa Tatjana
Malek wa Ujerumani kwa 5-7 6-4 6-4.
Licha
ya kutupwa nje ya mashindano, bingwa mara tano wa Wimbledon Venus
alisema; "Nilijihisi Marekani kwa mara ya kwanza " kutokana na aina ya
sapoti aliyooneshwa na kutoka kwa mashabiki wa nyumbani kwenye Uwanja wa
Arthur Ashe.
"Hii
ni mara ya kwanmza ambayo nimecheza hapa na kuona kundi kubwa la
mashabiki likiwa nyuma yangu kama hivi. Nilisubiri uungwaji huu kwa muda
mrefu, hatimaye nimeupata ingawa matokeo hayakuwa mazuri," alisema
Venus.
"Ilikuwa
ya kushangaza sana. Nilijisikia kama niliyeshinda dhahabu. Kiukweli
ilimaanisha kitu. Kwa sasa naangalia mbele kuona namna navyoweza kutumia
ipasavyo sapoti mara mbili yah ii niktakayopata katika michuano ya
mwaka ujao nikiwa bora zaidi."
No comments :
Post a Comment