Bondia
Manuel Charr wa Ujerumani akiokolewa na mwamuzi baada ya kupigwa na
Vitali Klitschko na kuchanika jichoni na kutokwa damu nyingi kama
anavyoonekana.
MOSCOW, Russia
Manuel
Charr, ambaye alshinda katika raundi kama hiyo alipoumana na Danny
Williams, juzi alilazimika kutoendelea na pambano lake dhidi ya Vitali,
kutokana na konde zito lililomchana juu ya jicho lake la kulia
BINGWA wa WBC Vitali Klitschko, alifanya
kazi rahisi ulingoni kumuwezesha kuibuka na ushindi pasipo changamoto
kubwa kutoka kwa Mjerumani Manuel Charr, katika dakika ya mwisho ya
raundi ya nne jijiji hapa.
Klitschko, 41, ameibuka mbabe wa pambano hilo dhidi ya mpinzani wake ambaye hakuwahi kupigwa huko nyuma.
Charr, ambaye alipata ushindi wa raundi
kama hiyo alipoumana na Mwingereza Danny Williams, alilazimika
kutoendelea na pambano hilo kuokana na konde zito lililomchana juu ya
jicho lake la kulia na kumsababishia kumwagika kwa damu nyingi.
Hata hivyo Charr alikuja juu kupinga
maamuzi – kufuatia majibu ya uchunguzi wa madaktari kuwa alikatwa na
kitu na kwamba jeraha lake halikutokana na ngumi, hivyo kupinga matokeo.
Klitschko kwa mara nyingine anaingia katika
ushindi wa utata, baada ya Februari mwaka huu kumchapa Dereck Chisora
kwa pointi, na kusababisha mgogoro baina yam kali huyo na David Haye
wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Haye, ambaye alipigwa kwa pointi na ndugu
wa kuzaliwa wa Vitali, Wladimir mwaka jana, alifanikiwa kumchapa Chisora
KO Julai mwaka huu nma kuamua kuomba pambano dhidi ya mkongwe huyu
Vitali.
Pambano baina ya Haye na Vitali, linaweza
tu kufanyika kama raia huyo wa Ukraine atashindwa uchaguzi wa nchi yake
ambako anawania ubunge, ambapo kama akishinda atalazimika kustaafu
masumbwi.
No comments :
Post a Comment