TIGO YASABABISHA KIZAZAA KWA WATEJA WAKE
Na Mwandishi Wetu
KUKATIKA kwa mawasiliano katika mtandao wa Tigo kwa wateja wake wote 
nchini kumezua kizazaa cha kuhaha kuwasiliana na ndugu zao na wengine 
kushindwa kutuma fedha kwa njia ya simu Tigo Pesa kutoka jana usiku hadi
 saa tano ya leo.
Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Tigo, Tuli Mwaikenda alisema tatizo hilo 
limetokana na kukatika kwa umeme uliosababisha mfumo wa mawasiliano ya 
Tigo kukatika na kusababisha usumbufu mkubwa.
Msemaji wa Kitengo cha Mawasiliano wa TANESCO, Badra Masoud alikiri 
umeme kukatika na hiyo imesababishwa na mitambo ya gesi inayozalisha 
umeme katika kisima cha Songosongo mkoa wa Lindi kupokea gesi chini ya 
asilimia 50.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. 
Fadhil Kilewo alisema kukatika kwa umeme kunatokana na uchakavu wa 
mitambo ya TANESCO.
 
 
 
                        
                    
 
  
 
 
 
No comments :
Post a Comment