Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi 
cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii  Tanzania (TTB)  
kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria wakati wa 
uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa (Malaria Safe 
Companys)  uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam 
jijini dar es salaam usiku huu ambapo Wizara ya afya inashirikiana na 
pamoja na taasisi za kimataifa na  Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta 
ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri
 wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey 
Meena baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania 
(TTB).
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi 
cheti Mzee  CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama
 ya  mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.
Waziri
 Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni 
na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara 
baada ya uzinduzi huo.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza 
na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili
 kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua 
rasmi kampeni ya kupambana na Malaria inayoitwa "Malaria Safe Companys" ,
 kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Raymond Mushi.
Waziri
 Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza 
na Rais Washirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Leodger Tenga 
wakati alipowasili katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam  kwa 
ajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria, kushoto
 ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.
Wadau
 waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa 
malaria kutoka kulia ni Mkurugenzi wa michezo katika Wizara ya Habari, 
Vijana , Michezo na Utamaduni Bw. Leonald Thadeo, Assah Mwmbene 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Mbunge wa Jimbo la Temeke Mh. 
Abbas Mtemvu na Mbunge na Waziri wa zamani Mh. Chrisant Mzindakaya.
Mkurugenzi wa Sahara Media Bw. Samwel Nyala kushoto akiwa na wadau wengine katika uzinduzi huoHyatt Regency Dar es Salaam.
Waziri
 Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiandika kitu huku Waziri wa Afya na Ustawi wa 
Jamii Mh. Hussein Mwinyi akipiga makofi katika uzinduzi huo.
Meneja
 Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim Mohamed Abeid Bakhressa akitoa 
ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika viwanda vyao.
Rais
 wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini  TFF Bw, Leodger Tenga 
akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jinsi sekta ya michezo 
ilivyosaidia kutokomeza malaria nchini.
Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab 
Khadija Kopa pamoja na kundi lake wakitumbuiza katika hafla hiyo 
iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam 



No comments :
Post a Comment