Meneja wa
Swahili Fashion Week, Washington Benbella akizungumza na waandishi wa
Habari wakati wa uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2012. Kutoka kushoto
ni Hassan Mrope, Meneja Mahusiano wa Swahili Fashion Week, Happy Shame
Meneja Masoko EATV..JPG
DAR ES SALAAM, Tanzania
Onyesho
kubwa la mitindo la Afrika Mashariki na kati linarajiwa kufanyika siku
tatu mfululizo katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia tarehe 6, 7 na 8
Desemba, 2012 ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.
Swahili
Fashion Week 2012 kwa ujumla itakutanisha pamoja wadau 50 katika tasnia
ya Mitindo kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na nyengine kuweza
kuonyesha ubunifu wao na kutoa mustakabali wa mwenendo wa tasnia ya
mitindo katika ukanda huu.
“Mwaka
tumekuwa kwa kiasi kikubwa, wabunifu 23 kutoka Tanzania wataweza
kuonyesha ubunifu wao na wengine waliobaki ni kutoka nje ya Tanzania,
ambao wote wataonyesha ubunifu wao katika jukwaa moja ukiachilia
wabunifu 16 walionyesha ubunifu wao katika maonyesha ya Swahili Fashion
Week yaliyofanyika Nairobi, Kenya, Oktoba 6, 2012” Alisema Meneja wa
Swahili Fashion Week, Washington Benbella
Katika
kuongeza maonyesho ya mitindo, mwaka huu Swahili Fashion Week shopping
Festival ambayo ilianza 2010 itakuwepo tena kwa mara nyengine ambapo
itashirikisha zaidi ya waonyeshaji 30 katika sehemu moja ikiwa ni kwa
ajili ya kuonyesha na kuuza bidhaa za ubunifu hivyo kuifanya kuwa msimu
mkubwa manunuzi ya kazi za ubunifu wa mitindo hapa Tanzania.
Kama
ilivyo ada, Swahili Fashion Week inatoa nafasi kwa kuendeleza vipaji,
ambapo tarehe 24 Novemba, 2012 kutakuwa na mchujo wa wazi kwa
wanamitindo wapya na wanaochipukia kwa jinsia zote, na mnamo tarehe 7
Desemba, 2012 kutakuwa na warsha kwa ajili ya wabunifu wote Tanzania
chini wadhamini wakuu wa warsha hiyo USAID Compete ambayo itafanyika
katika Hotel ya Golden Tulip” Aliongeza Benbella
Mashindano
tofauti yamepangwa kufanyika wakati wa Swahili Fashion Week, ikiwemo
Shindano la kumtafuta Mbunifu Bora anaechipukia na Mbunifu Bora wa
kubuni Fulana. Sio tu inatoa changamoto na ari ya ushindani katika
tasnia ya ubunifu nchini Tanzania, bali pia inaweka msingi imara kwa
wabunifu wa baadae.
“Sherehe
maalum za kufungua Swahili Fashion Week zinarajiwa kufanyika siku ya
Jumapili tarehe 25 Novemba, 2012, Thai Village kuanzia saa 9 usiku.
Sherehe hizo pia zitafuatiwa na kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa
kushindania tuzo mbalimbali zilizowekwa katika vipengele 16, tuzo hizi
ni za kwanza na ndio pekee katika ukanda huu. Tiketi za sherehe za
uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2012 zinapatikana sehemu zifuatazo,
Thai Vilage, Mgahawa wa Epidor uliopo Masaki, na Tanzania Mitindo House”
Alisema Meneja Uhusiano, Hassan Mrope
“Tukiwa
na mipango yenye ndoto za kutangaza biashara ya mitindo katika ukanda wa
Afrika mashariki na kati, ninapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru
washirika wetu pamoja na wadhamini wetu ambao karibia ya wote wamekuwa
wakitusaidia kutokea maonyesha yaliyopita mpaka sasa. Pia tuwashukuru
sana watu wote wanaosaidia tasnia ya mitindo hapa Tanzania kwa si tu
kuhudhuria matamasha na maonyesho kama haya bali pia kwa kununua bidhaa
zinazotengenezwa hapa nchini kwani hii inatangaza kinachotengenezwa
Africa “Made in Africa”. Alimalizia Benbella
No comments :
Post a Comment