Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene 
Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha 
kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na 
kushoto ni  DJ wake Athur Baraka. 
**************** Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakiwa na 
balozi wake Ambwene Yessaya “AY” leo wamewashukuru watanzania kwa 
kumpigia kura msaani maarufu wa kizazi kipya Ambwene Yessaya  “ AY “  na
 kumwezesha kuibuka mshindi wa tuzo ya kwanza katika kipengele cha Most 
Gifted East African video of the Year kupitia kibao chake kipya 
kijulikanacho kama “   I don’t wanna be alone”
  Akiongea na 
wandishi wa habari katika Ofisi za Airtel leo AY amechukua fulsa 
kuwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kuweza kumwezesha kuibuka na
 ushindi. Aidha alivishukuru vyombo vya habari kwa kuendelea 
kushirikiana naye katika kufikisha habari na kumsaidia kupata tuzo hiyo.
  Naye
 Afisa uhusino wa Airtel Jane Matinde alisema” tunafurahi kuona msanii 
AY ambaye ni balozi wetu kuibuka na tuzo iliyoshirikisha wasanii 
mbalimbali toka  Afrika, sisi tunasikia furaha kuona mafanikio ya 
wasanii wetu nchini yakiendelea kukua na ndio sababu leo tuko hapa 
kusherehekea ushindi  huu kwa pamoja na kuwashukuru watanzania kwa 
kumuwezesha AY kupata tuzo hii kwa kura zenu.
  Tunapenda pia 
kuchukua fulsa hii kuwaalika watanzani na wateja wetu leo pale nyumbani 
lounge usiku kuanzi saa tatu tuweze kujumuika na AY na kumpongeza kupata
 tuzo hii. Tutakuwa na wasanii wengi pamoja na wadau mbalimbali wa 
Musiki na pia utapata muda kupiga picha na msanii huyo na Tuzo yake 
 | 
No comments :
Post a Comment