Balozi wa kinywaji cha Hennessy Cyrile Gautier Auriol,  akizungumza
 na waandishi wa habari jana kuhusiana na mikakati yake ya kufanya 
mazungumzo na wafanya biashara mbali mbali wa hapa nchini.  Picha/ Mpiga Picha Wetu.
*************************** 
Na Mwandishi wetu
Balozi
 wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, yupo nchini kwa ajili 
ya shughuli mbali mbali pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa jiji la
 Dar es Salaam.
Auriol
 aliwasili jijini juzi na kufanya mazungumza na wenyeji wake kabla ya 
kuelezea nia ya safari yake ambayo lengo kubwa ni kutanua soko la 
kinywaji hicho maarufu duniani kwa Watanzania nan chi za Afrika 
Mashariki.
Alisema
 kuwa pamoja na kukutana na wafanyabiashara, pia atakutana na watu wa 
sekta tofauti, miongoni mwao ni wanamuziki na wanamitindo.  Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku tano.
Alifafanua
 kuwa ujio wake ni mara ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ameona
 kuna mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara na hasa katika soko la 
vinywaji vikali.
Alisema kuwa kinywaji cha Hennessy kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja kwa Watanzania kuanza
 kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya bora. Ikiwa na zaidi 
ya historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa kinywaji (Cognac) bora 
zaidi duniani.
Pia Auriol
 atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu 
ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi 
ya wanawake watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya 
kinywaji cha Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji 
hicho lengo likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji 
hicho wakiwa majumbani mwao.
Balozi
 Auriol pia atahudhuria chakula cha jioni na wafanyabiashara wa hapa 
nchini katika mgahawa wa Akemi uliopo katika ghorofa la Diamond Jubilee.
 Balozi Auriol atatoa elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na uonjaji wa 
kinywaji hicho pamoja na chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa 
hotel hiyo.
Ziara
 ya balozi Auriol inaenda sambamba na juhudi nyingine za kutangaza 
kinywaji hicho hapa nchini, mojawapo ikiwa ni kampeni ya mabango ya 
‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa jiji zima pamoja na ukamilishaji wa 
chumba cha Hennessy kilicho katika Club 327, ambacho balozi Auriol 
atakizindua.
Balozi
 Auriol atakuwa na kikao maalumu pia na wapenzi wakubwa wa kinywaji 
hicho, na pia atawazawadia mialiko maalumu ya kuingia kwenye klabu ya 
wapenzi wa kinywaji hicho ya Afrika mashariki.
Pia
 atatoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa 
za jijini. Lengo kuu la mafunzo hayo yatakayofanyika katika hoteli ya 
Southern Sun na George & Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi 
utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati 
wakiburudika na kinywaji cha Hennessy kwenye bar au hotel 
wanazozipendelea.
No comments :
Post a Comment