Mwenyekiti wa Simba,
Ismail Aden Rage akizungumza na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wa tawi la Wekundu
wa Terminal Ubungo jijini Dar es Salaam leo. (Picha na habari Mseto Blog)
Baadhi ya wanachama wa tawi hilo wakimsikiliza Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage
Akuffo, Ochieng kwa heri Simba
.Rage
amwaga cheche, amrejesha Hanspope
.Amtangaza rasmi Julio, Prof Maji
Marefu naye aula
Na Clezencia Tryphone
WAKATI
mzimu wa kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu Bara mabingwa watetezi Simba, ukiwa
unaiandama klabu hiyo, Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage ametangaza kuachwa kwa
nyota wa kimataifa, Daniel Akuffo na Paschal Ochieng.
Rage
aliyabainisha hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wanachama
wa Tawi la Simba la Wakali wa Terminal ‘Mwanzo Mwisho’ kuhusiana na mustakabali
wa klabu hiyo ambayo hivi karibuni ilikumbwa na mtafaruku kutokana na kumaliza
mzunguko wa kwanza wa ligi ikiwa nafasi ya tatu, baada ya kuongoza kwa muda
mrefu.
Mwenyekiti
huyo alisema, tayari wamemalizana Mghana Akuffo huku wakiwa katika mchakato wa
mwisho kumuondoa Ochieng. Nyota hao ambao walisajiliwa msimu huu, wameshindwa
kuonesha uwezo.
Pia
Rage ambaye hivi karibuni alizifuta Kamati ndogondogo zote, alisema, amemteua
Zakaria Hanspope kuwa Mwenyekiti Kamati ya Usajili akisaidiana na Mbunge wa
Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarifi kama,
Profesa Majimarefu, huku wajumbe wakiwa ni wafanyabiashara maarufu, ili waweze
kuiinua Simba. Alimsifu Hanspope, kwa kujitolea fedha zake mfukoni bila ya
kuhitaji kutajwa.
Mwenyekiti
huyo, pia alifafanua kuwa, alimuomba radhi Nahodha wa timu hiyo, Kipa Juma
Kaseja kwa kitendo cha mashabiki kumtukana katika mechi na Mtibwa ambayo
walilala 2-0 na kuwa, hawana mpango wa kumuondoa labda atake yeye kwanza, kwani
licha ya kuwa mchezaji wao ni mwanachama halali wa Simba na ana kadi ya
uanachama.
Aliwaeleza
wanachama hao kuwa, pia wamefanya mabadiliko benchi la ufundi, ambako Jamhuri
Kihwelu ‘Julio’ atakuwa Meneja na Kocha Msaidizi pamoja na Mganda Amate, huku
kuhusiana na Kocha Mkuu akidai atalizungumza siku nyingine, ambako wanachama
wakadakia wakisema, tunamtaka Babu asiondoke, huku Rage akijibu Simba oyee na
wanachama hao kuitikia tano bila.
Rage
ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini, alitamba kuwa, mzunguko ujao watampiga
mtani wao Yanga, ‘hamsa’ kama sio sita.
Kuhusiana
na klabu kujiendesha, alisema inatumia sh mil 50 kwa mwezi kwa ajili ya
mishahara na kuwa, mdhamini hatoi hata nusu yake na kuwa, Simba ina uwezo wa
kujisimamia kwa asilimia 92, kwa kuwa toka wameingia madarakani Mei 31, 2010
walikuta haina umeme, madirisha na wao wamehakikisha wamelipa na kuweka vioo
vya giza, ‘tinted’ na kwa sasa wameboresha maduka yao.
Akilizungumzia
Tawi la Mpira Pesa, ambalo linataka mkutano wa dharura,
Alisema,
kwa wameamua kumwaga ugali wao wamemwaga ugali, ambako limesimamishwa kwa miaka
miwili ili waweze kuwa na nidhamu zaidi watakaporejea na kusisitiza hakuna tawi
lolote ambalo liko juu ya klabu.
No comments :
Post a Comment