Miss East Africa France Fiona Ruboneka (24)
Warembo mbalimbali wanaoishi Ulaya na 
walioshinda katika mashindano ya Miss East Africa huko Ulaya pia 
watashiriki katika mashindano ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika 
tarehe 07 December katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam 
warembo hao ni:
   1. MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
2.      MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
3.      MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24)
Fainali za 
mashindano ya Miss East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi 
za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea,
 Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na 
Mauritius.
Mashindano ya 
Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni 
ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet 
ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga 
umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa 
Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam 
Imeandikwa na kusainiwa na,
Rena Callist,
EXECUTIVE PRODUCER
MISS EAST AFRICA BEAUTY PAGEANT


No comments :
Post a Comment