Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania
Bw. Peter Fauel, akitangaza Punguzo la Asilimia Kumi ya Malipo ya mwezi
kwa wateja wa Televisheni kwa Vipindi vya DStv likaloanza hapo kesho,
ambapo amesema punguzo hilo litawawezesha wateja wao kulipia huduma za
Matangazo ya Televisheni ya kituo hicho kwa gharama nafuu. Pia amesema
Offer hiyo ya Punguzo la bei ni hatua ya Kampuni hiyo kurudisha fadhila
kwa wateja wake kuelekea katika kipindi cha maadhimisho ya sikukuu za
mwisho wa mwaka. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice
Barbara Kambogi na Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Bi. Furaha
Samalu.
Meneja Masoko wa Multichoice wa
Kampuni hiyo Bi. Furaha Samalu akitoa ufafanuzi kuwa katika kipindi hiki
cha kuelekea matumizi ya mfumo wa Digitali DStv kwa kuwajali wateja
wake imepunguza gharama za kuunganishwa ambapo sasa ni kwa shilingi za
Kitanzania 169,000 unaweza kusheherekea msimu wa sikukuu na DStv.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multchoice Barbara
Kambogi (wa pili kushoto) akiwahakikishia wateja wa DStv kuwa sasa
kampuni hiyo imezidi kuboresha huduma zenye viwango vya hali ya juu na
kuwataka wazazi kutumia fursa hii ya punguzo la bei ya kuunganishwa ili
watoto wao waweze kushuhudia vipindi mbali mbali vya kuelimisha na
kuburudisha ikiwemo filamu kali, katuni maridadi, michezo mbalimbali
katika kipindi hiki cha likizo kwa watoto wao na kuwa huu ndio sasa muda
muafaka kwa kujipatia DStv.
Meneja
Mauzo wa DStv Tanzania Bw. Salum Salum akifafanua kuwa Multichoice
imepanua wigo wa kutoa huduma kwa wateja ambapo sasa wanamawakala 200
nchini na kuwataka wanapokwenda kulipia Ving'amuzi vyao ni lazima
wahakikishe vimewashwa ili kurahisisha kufanyika kwa huduma hiyo pia
amesema wateja wa DStv wanaweza kufanya malipo ya huduma hiyo kupitia
simu za mkononi na ukizingatia kampuni hiyo imeongeza maeneo ya kutoa
huduma ikiwemo Uchumi Super Market, Kariakoo na Mlimani City kwa wakazi
wa Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment