Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 7, 2012

KHADIJA KOPA ALIVYOFUNIKA MITIKISIKO YA PWANI DAR LIVE



Malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa, kutoka T.O.T akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria Mitikisiko ya Pwani Dar Live Jumamosi. MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa, juzi (Jumamosi) alifunika vilivyo katika Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lililofanyika ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.


Khadija Kopa na vijana wake wakiwa wameiteka Dar Live kwa burudani. Tamasha hilo lilipambwa na makundi mbalimbali ya taarab yakiwemo Jahazi, Coastal, TOT na mengineyo. Watangazaji mahiri kutoka Times Radio wakiongozwa na Gardner G Habash na Khadija Shaibu 'Dida' walinogesha tamasha hilo na kulifanya liwe la kipekee.


Kiongozi wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf 'Mfalme', akiimba na mashabiki wake.

Mke wa Mfalme, Leila Rashid, akilipamba Tamasha la Mitikisiko ya Pwani ndani ya Dar Live.

Mwanahawa Ally wa East African Melody akiwarusha mashabiki wa Mitikisiko ya Pwani.

Kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhan 'Isha Mashauzi', akiwapa raha mashabiki.

Maua Tego wa Coastal Modern Taarab akiwa stejini.

Sehemu ya mashabiki waliofurika Dar Live kushuhudia tamasha hilo.

Khadija Kopa na wasanii wenzake wa TOT wakilitawala jukwaa.

Wasanii wa TOT wakizidi kunogesha tamasha hilo.

Mzee Yusuf akimchombeza mkewe, Leila Rashid.

Mashabiki wa Arsenal nao walikuwepo.

Wapenzi wa taarab waliokuwa VIP wakifuatilia tamasha hilo.

Isha Mashauzi akionyesha mbwembwe zake stejini.

Mashabiki waliopanda stejini kumtunza Mzee Yusuf wakijiachia kwa raha zao.

Nyomi iliyohudhuria Tamasha la Mitikisiko ya Pwani.

No comments :

Post a Comment