Tigo yashika nafasi ya 5 duniani na ya kwanza 
Afrika kwa makampuni ya simu katika  kujitoa kwa huduma za mitandao 
ya kijamii, hii ni kulingana na matokeo yaliyotolewa jana na kampuni  
ya ‘Socialbakers’ inayohusika na masoko, ufuatiliaji na upimaji 
wa mitandao ya kijamii duniani. 
Tigo Tanzania ina wastani wa kujibu wa dakika 24 na kiwango 
cha majibu ya 87.49% dhidi ya kiwango cha dakika 520 na kiwango cha 
65.50% kiwango cha kujibu, kwa sekta hii. Makampuni au bidhaa ambazo 
zinajitoa kwa huduma bora za mitandao ya kijamii  zinaonekana kuwa na 
huduma bora kwa wateja.
“Tunajivunia  kuweza kushika namba 5 bora kwa 
operasheni  zetu duniani na kuwa bora zaidi kwa Afrika.Hili inaonyesha 
wazi  juhudi na nguvu tunazoweka ili kuhakikisha kuwa tunaongea 
na kuwasikiliza wateja wetu wakati wote, kwa njia inayokwenda na wakati 
wa sasa, alisema, Diego Gutierrez Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo 
Tanzania”.
Huduma za kijamii kwa wateja na vipimo vyake ni pamoja 
na idadi ya mashabiki,idadi ya maswali yanayoulizwa na mashabiki wa 
kurasa,muda wa majibu,wastani wa muda ambao kampuni inachukua kujibu 
maandiko ya watumaji na kiwango cha majibu au asilimia ya wanaopata 
majibu kutoka kampuni hiyo.
Kwa sasa Tigo Tanzania imefikisha mashabiki 110,000 
wa Facebook na kuwa mtandao unaoongoza kwa kuwa na wafuasi wengi facebook.
Socialbakers ni moja kati ya kampuni kubwa zinazofanya tathmini 
ya mitandao ya kijamii duniani na lengo lake kubwa ni kufuatilia na 
kupima muonekano ya mitandao, katika kila lengo la mtandao dunia nzima 
pale ilipo. Socialbakers pia ni moja kati ya kampuni za kuendeleza masoko 
zinazotumiwa na Facebook .

No comments :
Post a Comment