Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, 
Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na mmoja  wa wajasiliamali aliyeshinda 
shindano la Tigo Reach For Change, Bi.  Brenda D. Shuma pamoja na 
Mkurugenzi wa Reach For Change Sarah Damber.
Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, 
Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na washindi  watatu wa shindano la Tigo 
Reach For Change,  Bi. Brenda D. Shuma,  Nyabange Chirimi na Thadei 
Msumanje, kulia ni Mkurugenzi wa Reach For  Change Bi.  Sarah Damber.
 Mmoja wa wajasiliamali aliyeshinda 
shindano la Tigo Reach For Change,  Bi. Brenda D. Shuma akielezea jambo 
kwa waandishi wa Habari.
Meneja wa Tigo, kitengo cha huduma za
 Jamii Woinde Sishael akifafanua  jambo mbele ya waandishi wa habari na 
wadau walihudhuria mkutano huo. 
---
Mwezi
 Septemba mwaka  huu, Tigo kwa kushirikiana na Shirika la kujitolea la 
Reach For Change  kwa mara ya kwanza nchini Tanzania walizindua programu
 iliyodhamiria  kutambua na kuendeleza mawazo madhubuti ya 
wajasiriamali  yenye  lengo la kuboresha maisha ya watoto.  
Baada ya kampeni ya mwezi mmoja ya 
kutoa wito kwa watanzania wote  wenye mawazo madhubuti kujitokeza kwa 
ajili ya ajili ya kuwasilisha  maombi yao, tulipokea maombi 2480, ambapo
 waombaji 15 walifika fainali   ikifuatiwa na mchujo mkali ambao 
ulijumuisha wafanyakazi wa Tigo na  Reach For Change pamoja na wataalamu
 wengine wa nje. Hawa waliendelea  kuchujwa hadi tulipofanikiwa kupata 
washindi watatu  baada ya mawazo  yao kupitishwa na jopo la majaji.
"Mpango wa kurejesha kwa Jamii sehemu
 ya faida yetu, ni moja  ya nguzo ya kampuni yetu na tuna nia ya dhati 
na mpango huu wa Reach  for Change, ambao ni sehemu ya mpango wetu 
kimataifa. Tigo Tanzania  imepokea maombi yenye mvuto na ushindani wa 
hali ya juu. Washindi wa  nafasi tatu za juu ambao wamechaguliwa leo si 
tu walishinda mioyo za  majaji bali waliwavutia na ubunifu wa mipango 
yao dhubuti. Sasa waanapokea  ufadhili wa $25,000 kama mshahara wa 
mwaka, kwa miaka mitatu mfululizo  ili kuweza kuzingatia na kutimiza 
malengo yao," alisema Andrew  Hodgson, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tigo. 
Washindi wa shindano la wajasiriamali
 la Tigo Reach For change mwaka  2012 ni Brenda-Deborah  Shuma, Nyabange
 Chirimi na Thadei Msumanje. Miradi yao watakayo ianzisha italenga 
katika  kuwawezesha watoto wenye ulemavu na vijana wenye ujuzi wa 
kiufundi,  kusaidia elimu ya watoto wa mitaani na kuboresha elimu 
kupitia Teknolojia  ya Habari na Mawasiliano (ICT).
'Tigo Reach for Change' imelenga katika kuainisha na kusaidia wajasiriamali  kwenye miradi ya kijamii
 na wenye mawazo yakinifu juu  ya kuboresha maisha ya watoto wa 
Tanzania. Washindi hawa watatu sasa  wanajiunga na programu ya miaka 
mitatu ya kuboresha miradi yao, ambapo  mawazo yao yatabadilishwa kuwa 
miradi endelevu. Mbali na hayo, watapata  mshahara wa dola 25,000 kwa 
mwaka kwa miaka mitatu mfululizo pamoja  na  ushauri wa kitaalamu kutoka
 kwa wafanyakazi waandamizi wa Tigo.
Reach for Change ni  Shirika la 
kujitolea lililoanzia Sweden ambalo lilianzishwa na Kinnevik,  ambaye 
ndiye aliyeunda kampuni ya Millicom (shirika anzilishi la Tigo).  
Kampeni ya kutafuta wajasiriamali kwa mkakati wa Reach for Change kwa  
mara ya kwanza ulianzia huko Sweden mwaka 2010 ikifuatiwa na Russia  
2011 kabla mwaka huo huo kuanzishwa barani AfriKa katika nchi ya Ghana. 
 Hadi sasa imeweza kuboresha maisha ya watoto wapatao 140,000 nchini  
Ghana.
Tigo
 na Reach For Change  imeanza rasmi utafutaji wa wajasiriamali kwenye 
miradi ya kijamii,   katika nchi zinazotoa huduma yake barani  Afrika, 
kwa kuzinduliwa  kwanza Rwanda ikifuatiwa na Tanzania, halafu Ghana,  
Congo DRC, Senegal  na mwishomi itakuwa Chad miezi michache ijayo.





No comments :
Post a Comment