Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 14, 2012

HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) YAFANYA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA




Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012. 
 
  Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa  na Mwenyekiti wa ChaCha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Ambapo Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo  Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na  Mhe. Abdulrahaman Kinana.

 Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;

    Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
    Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Mhe. Vuai Ali Vuai.
    Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
    Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
    Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
    Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.


 Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.

No comments :

Post a Comment