Waziri wa maliasili za Utalii Balozi
Khamis Kagasheki akihojiwa na kituo cha Televisheni ya Taifa TBC mara
baada ya kutembelea mabanda ya makampuni ya Tanzania yanayoshiriki
katika maonyesho ya Utalii ya World Travel Market yanayoandaliwa na
kufanyika katika eneo la Excell jijini London nchini Uingereza,
yakishirikisha makampuni mbalimbali ya utalii kutoka pande zote za
dunia, Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni zaidi ya 55 yakiwa
chini ya Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB).
Waziri Balozi Kagasheki
amesifushiriki wa makampuni ya Tanzania katika maonyesho hayo lakini
amesisitiza kwamba makampuni hayo yaongeze juhudi za kutangaza utalii wa
Tanzania mpaka kufikisha lengo la idadi ya watalii milioni moja kila
mwaka, ameongeza kwamba kuna haja ya kuongeza vitanda zaidi nchini
Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea katika mbuga zetu
na kufanya utalii kuka zaidi, Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi kesho.
Fullshangweblo iko jijini London nchini Uingereza ikikumuvuzishia matukio haya moja kwa moja kutoka katika maeneo ya Excell ambako ndiko maonyesho hayo yanafanyika.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri aliasili na Utalii wa Balozi
Khamis Kagasheki akisalimiana na Issa Ahmed Othman Mshauri wa Rais
masuala ya Utalii Zanzibar wakati alipotembelea banda la Tanzania katika
maonyesho ya utalii ya (WTM) jijini London leo nchini Uingereza
Waziri Balozi Khamis Kagasheki
akizungumza na Leila Ansel Mkuu wa mauzo na masoko kampuni ya Tanzania
Zara Adventures wakati alipotembelea katika banda hilo leo kwenye
maonyesho ya utalii ya WTM nchini Uingereza.
Yvone Baldwin Afisa mauzo wa kampuni
ya ndege ya Precision Air akimkabidhi zawadi Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza Mh. Peter Kallaghe mara baada ya kutembelea banda hilo leo
akiongozana na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki.
Waziri wa Maliasili Balozi Khamis
Kagasheki akizungumza na Rashid Adam Meneja Masoko wa Tanzania Zara
Adventures wakati alipotembelea maonyesho ya Utalii ya WTM katika banda
la Tanzania leo jijini London, wa pili kutoka kushoto ni Mh. Peter
Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katikati ni mama Balozi.
Waziri Balozi Khamis Kagasheki
akizungumza na Laura Meneja wa Maendeleo ya Biashara kampuni ya Laitolya
Tours & Safari Ltd kushoto wakati alipotembelea banda la kampuni
hiyo kwenye maonyesho ya WTM leo, kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi
ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akiwahudumia
watu mbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania leo katika
maonyesho ya Utalii ya WTM jijini London Uingereza
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii ya
Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwa katika picha ya pamoja na
wakurugenzi wa African Environments Richard Beatty na Janice Beatty
katika maonyesho hayo.
Leila Ansel Mkuu wa mauzo na masoko
kampuni ya Tanzania Zara Adventures akizungumza na mmoja wa wageni
waliotembelea katika banda la kampuni hiyo katikati ni Rashid Adam
Meneja Masoko wa Tanzania Zara Adventures.
Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza akizungumza na mdau Juma Mabakila wakati akitembelea
banda la Tanzania kwenye maonyesho ya WTM
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii ya
Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwasikiliza wageni mbalimbali waliofika
katika banda la Tanzania katika maonyesho hayo leo.
Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili Utalii wa
pili kutoka kulia akizungumza na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB Devotha Mdachi mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania
katika maonyesho ya Utalii ya WTM nchini Uingereza , kulia ni Mh. Peter
Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katikati ni Mama
Balozi.
Mmoja wa washiriki kutoka kampuni ya
Africa Adventure akihojiwa na kituo cha televisheni cha TBC katika
maonyesho ya Utalii ya WTM yanayofanyika jijini London nchini Uingereza.
Waziri Balozi Khamis Kagasheki
akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wakati
alipotembelea maonesho hayo kushoto ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya
Utalii nchini TTB.
Washiriki mbalimbali wakiwa katika
banda la Tanzania wakipokea wageni mbalimbali wanaotemelea kwenye banda
hilo kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu utalii wa Tanzania.
No comments :
Post a Comment