MWIMBAJI maarufu wa
muziki wa Injili nchini, Rose Muhando na mwenzake Enock Jonas (Zunguka)
wanatarajiwa kutia chachandu katika tamasha la kwanza kubwa kufanyika Mkoani
Kagera.
Tamasha hilo la Shangwe Kagera
lina lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na
wanaoishi katika maisha magumu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta
anasema kuwa matayarisho ya tamasha hilo yanaendelea vizuri kutokana na
mwitikio mkubwa wa watu mbalimbali waliojitokeza kushiriki.
Pia, Mutta anasema bendi
ya muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya
wanakwaya wa makanisa mbalimbali, kikundi cha watoto yatima wanatarajia pia
kutumbuiza.
Mutta anasema tamasha
hilo la aina yake linatajiwa kufanyika Uwanja wa Kaitaba na pia kwenye ukumbi
wa Lina’s mjini Bukoba, siku ya Uhuru, Desemba 9.
“Mpaka sasa
tumekamilisha sehemu kubwa ya matayarisho hayo ikiwamo kulipia uwanja pamoja
sehemu ya malipo kwa wasanii ambao watashiriki,” alisema.
Pia, mkurugenzi huyo
aliwaomba wadhamini zaidi na wadau wengine wa maendeleo na watoto kujitokeza
kushiriki ili kuwasaidia jamii hasa watoto yatima na wengine wanaoishi katika
mazingira magumu.
Lengo la Tamasha:
Ni kuhamasisha jamii
kuishi kwa amani,kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza kimaisha
ili na wao wajione ni sehemu yao.
Katika kutambua hilo
kampuni yetu iliamua kufanya utafiti mdogo nakugundua changamoto nyingi katika Mkoa
wa Kagera, mojawapo ni kuwa na watoto wengi wanaoishi katika mazingira magumu.
Baada ya kuliona hili, tulitembelea vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao,
mojawapo ni Tumaini Children’s Centre kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili
la Ki lutheri Tanzania (KKKT).
Kituo hiki kinalea
watoto wote bila kujali kabila,jinsia wala dini zao, kwa sasa kituo hiki
kinahudumia watoto zaidi ya 800, kwa kuwapatia elimu,chakula, malazi n.k ambapo
kwa muda mrefu kimekuwa kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa wametangaza
kuusitisha kwa maelezo kuwa jamii ya Watanzania inapaswa kujifunza na kuanza
kuhudumia watu wao wenyewe.
Kutokana na hilo ndiyo maana tumeonelea tuwe na tamasha la kuamasisha jamii ili ianze kuona umuhimu wa kusaidia wenzao wanaohitaji msaada.
No comments :
Post a Comment