Wanamuziki
wa bendi ya Mashujaa, wakiongozwa na Chalz Baba (katikati) wakijifua
wakati wa mazoezi yao ya maandalizi ya uzinduzi wa Albam yao ya pili
inayokwenda kwa jina la Risasi Kidole, uzinduzi unaotarajia kufanyika
kesho katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, huku ukisindikizwa na
mwanamuziki mahiri kutoka Congo, JB Mpiana.
Kiongozi wa bendi hiyo, Chalz Baba, akiongoza mashambulizi wakati wa mazoezi hayo ya maandalizi leo.
************************
BENDI
ya Mashujaa kesho siku ya Ijumaa itazindua albamu yake ya pili
ijulikanayo kwa jina la Risasi Kidole pamoja na bendi maarufu ya Congo,
Wenge BCBG iliyochini ya mwanamuziki JB Mpiana kwenye viwanja vya Leaders club, Kinondoni.
Uzinduzi
huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku na maandalizi yake yamekwisha
kamilika kwa mujibu wa meneja wa bendi ya Mashujaa, Martin Sospeter.
Sospeter alisema kuwa wamejiandaa vilivyo katika uzinduzi huo na lengo
lao kubwa ni kuweka historia katika muziki wa Tanzania.
Alisema
kuwa wamekaa kambini muda wa siki mbili na wameandaa vitu vingi vipya
kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa dansi nchini.
Alisema kuwa kuna rap ya Ua Mbu na Dume la Simba kutoka kwa marapa wao,
Saulo Ferguson na Sauti Radi.
Alifafanua
kuwa wanamuziki wake wameadhimia ‘kufunika’ katika uzinduzi huo kwani
anahistoria nzuri katika muziki wa Tanzania na kufanya kazi katika bendi
nyingi.
“Tunawaomba
watanzania waje waone nini tunakifanya mbele ya gwiji la muziki wa
dansi Afrika, JB Mpiana, najua wao wamepania, lakini sisi tumepania
vilivyo kusafisha nyoyo za mashabiki ambazo kwa sku nyingi hawajapata
burudisha la mioyo zao,” alisema.
Kiongozi
wa bendi hiyo, Charlz Baba alisema kuwa wamepania kutoa somo kwa
wanamuziki wa dansi hapa nchini ambao wamekuwa wakisubiri waone
watafanya nini. Alisema kuwa wameandaa nyimbo nyingi nzuri na wamepatia kutawala soko la muziki hapa nchini.
“Njooni
muone nini tunafanya katika muziki wa dansi, kambi yetu imekuwa nzuri
na mafanikio makubwa, naomba mashabiki waje kutuunga mkono nasi
tutawaunga mkono kwa kutoa burudani safi,”alisema Chalz.
Albamu
ya Risasi Kidole ina jumla ya nyimbo sita. Nyimbo hizo ni Umeninyima,
Tikisika, Hukumu ya Mnafiki, Ungenieleza, Kwa Mkweo na wimbo uliobebab
jina la albamu hiyo, Risasi Kidole
No comments :
Post a Comment