Waziri wa Fedha Dkt William
Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza mradi
wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani Uyui juu ya kuufanya
mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda
kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia. Waziri huyo
alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya
wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti
wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa
Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa
akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49
ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola jana wilayani
Uyui wakati Waziri huyo alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano
ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi
huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui Said Shaban Ntahondi na
kushoto ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na
wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia wa
Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
PICHA na GCU - HAZINA
No comments :
Post a Comment