Mkuu wa Mkoa Shinyanga Ali Lufunga (wakwanza mbele) akikata utepe
kuzindua tawi jipya la Benki ya Exim ya Tanzania mjini Shinyanga mwishoni mwa
wiki. Nyuma yake kushoto ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo Anita
Goshashy. (Na Mpiga Picha Wetu)
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
BENKI
ya Exim Tanzania imepiga hatua nyingine kwa kufungua tawi jipya mjini
Shinyanga ikiwa ni kutekeleza mpango wa benki hiyo wakufikisa huduma za
kibenki katika maenoe mbali mbali nchi.
Benki
hiyo kwa sasa imefikisha idadi ya matawi 25 nchi nzima huku ikitarajia
kufungua mwtawi mengine kwenye mikoa ya Tabora, Arusha and Dar es Salaam
kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa tawi hilo jipya mjini Shinyanga, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Exim ya Tanzania, Bw. Anthony Grant alisema kuwa
ufunguzi wa tawi hilo jipya unaonyesha dhahiri jitihada za benki hiyo
kufikisha huduma zakibenki kwa wananchi waliopo pembezoni mwa nchi.
Grant
alisema kuwa benki yake kwa sasa imejikita katika mpango wa kutanua
huduma zake wenye lengo la kuhakikisha kuwa benki inafungua matawi mapya
katika maeneo yasiyoweza fikiwa na benki nyingine kabla ya mwisho mwa
mwaka huu.
“Dhamira
ya Benki ya Exim ya kuongeza mtandao wa matawi yake unaonyesha jitihada
ya benki yetu kufikia wananchi wengi nchi nzima. Tunafuraha sana
kufungua tawi hili mjini Shinyanga kwa kuwa linazidi kuimarisha huduma
zetu nchini. Tawi la Shinyanga ni uthibitisho wa jitihada zetu za
kufikisha huduma za kibenki karibu na watu.
“Mkoa
wa Shinyanga una vivutio vingi vya kibiashara na unahitaji huduma za
kibenki zilizobora; na kwa sababu hizo benki ya Exim itaendelea kuwekeza
kwenye tafiti mbalimbali ilikutoa huduma za kipekee zinazolenga makundi
mbali mbali hapa nchini,” alisema.
Grant
alisema benki yake imejikita katika kusaidia kukuza wafanyabiashara
wadogo na wakati (SMEs) nchini Tanzania kwa kuelewa kuwa biashara ndogo
ndogo na za kati ndiyo chachu ya kukuza uchumi endelevu.
“Biashara
ndogo ndogo za kati bado ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi nyingi
zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Benki ya Exim itaendelea kusaidia
wafanyabiashara wadogo na wakati nchini kupitia bidhaa/huduma maalum
zinazokidhi mahitaji yao,” aliongeza Grant.
Naye
Mkuu wa Mkoa Shinyanga Ali Lufunga wakati wa hafla hiyo aliwaasi
wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa mbali mbali zitakazopatikana na
ufunguzi wa Tawi la Benki ya Exim mjini Shinyanga.
“Uamuzi wa benki ya Exim kufungua tawi jipya mjini hapa ni ishara tosha kuwa benki hii ina imani na mkoa wetu.
“Wananchi, tuache mambo ya kizamani ya kutumia vibubu na tuanze utamaduni wa kuweka fedha zetu benki,” alisema Lufunga.
No comments :
Post a Comment