Wawakilishi
wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakigonganisha glasi za mvinyo
wa matunda ya Mananasi uliotengenezwa nchini Burundi wakati wa hafla
iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)kwenye maonyesho ya
utalii ya (ITB) yanayofanyika kwenye jengo la Mense Berlin jijini Berlin
Ujerumani, Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na mkakati wa Kutangaza
utalii wa Afrika Mashariki na mwaka huu ilikuwa na kazi moja ya kunadi
maajabu manne ya Afrika yaliyopatikana katika ukanda huu wa nchi za
Afrika Mashariki ambayo ni Mlima Kilimanjaro, Mto Nile, Mbuga ya wanyama
ya Serengeti na Ngorongoro Crater huku Tanzania ikiwa kinara kwa ukanda
huu wa Afrika Mashariki kwa maajabu yake matatu ambayo ni Mlima
Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na Ngorongoro Crater jambo lililofanya
itamkwe mara nyingi miongoni mwa viongozi waliopata nafasi kuzungumzia
utalii wa Afrika Mashariki PICHA NA FULLSHANGWEBLOG
Kaimu
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akipokea tuzo
maalum iliyotolewa na iliyotolewa kwa nchi za jumuiya ya Afrika
Mashariki kutoka kwa Bi Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda
katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye
maonyesho ya (ITB) Berlin jana, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki kulia anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu wa (EAC)
Jesica Eriyo
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Meena kulia akiwa na
Adolf Mchemwa Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania Ujerumani wakiwa
katika hafla hiyo
Bi.
Maria Mutagamba Waziri wa Utalii wa Uganda ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika hafla hiyo akisoma hotuba yake na kuzungumzia masuala mbalimbali
kuhusu utalii wa nchi za Afrika Mashariki
No comments :
Post a Comment