Mmiliki na Mwendeshaji wa Kipindi cha Ongea na Janet Bi. Janet Sosthenes Mwenda katika moja ya vipindi walivyofanya na Bondia maarufu nchini Tanzania Japhet Kaseba. |
Mmiliki na Mweneshaji wa kipindi cha ‘Ongea na Janet’ Bi. Janet Sosthenes Mwenda.
Sasa ‘Ongea na Janet’ inaonyeshwa katika Dstv kufuatia kuingia nao mkataba.
MO BLOG: Tulishuhudia
uzinduzi wa ‘Ongea na Janet’ tukaanza kuona vipindi vikienda hewani
hebu tuweke wazi yapi mafanikio uliyopata mpaka sasa..?
JANET: Mafanikio nilianza kuyaona kwenye vipindi 13 tu vya mwanzo ambavyo vilitengeneza ‘Season One’. Nashukuru
Mungu ‘Ongea na Janet’ ilijulikana haraka sana, ikapata watazamaji
wengi, ‘comments’ nazo zikawa nyingi, ‘changes’ zikawa nyingi nikajikuta
kila ninapokwenda siitwi tena Janet naitwa ‘Ongea na Janet’.
Hilo
lilikuwa ni fanikio la kwanza kwamba niliondoka kwenye media muda mrefu
na niliporudi nikapokewa vizuri kwa hiyo nawashukuru kwanza watanzania
wenzangu kwa hilo, nawashukuru sana mashabiki wa Janet kwa kunipa ‘love’
ukweli.
Lakini pia fanikio lingine lilikuja kujitokeza ambalo sikulitegemea kwa kipindi kile lilikuja kama ‘surprise’
kwangu kwani nikiwa sina hili wala line nikapata simu kutoka MNet-Dstv
Nairobi wakaniambia kwamba shoo yangu wameipenda na wataichukua, wakati
huo nikuwa nimesha ‘apply’ siku nyingi sana mpaka nimesahau.
Wakanipa na ‘amount’ nikakubali wakaniuliza unazo ngapi? Wakati huo ndio nimemaliza ‘Season One’ nikawaambia ziko 13 wakasema wangependa kama zingekuwa 26 nikasema sawa nitakaporudi ‘Season Two’ nitawapatia wakakubali.
Hivyo niliporudi ‘Season Two’ nikawa nimeingia kibiashara zaidi na Dstv wakawa wameni-‘support’ nikaweza kubadilisha set up nzima ya ‘Ongea na Janet’ na wakanipa hamasa zaidi na nikapata nafasi ya kuitangaza nchi yangu kwa na kwa sababu naoneka katika nchi nane (8) tofauti.
Pia nikagundua moja kwa moja kuwa sasa nimeingia kwenye ‘competition’ na watu nane wanaoziwakilisha nchi zao kwa maana ya kwamba Tanzania iko kwenye ‘competition’ ya ‘talk show’ na nchi nane za Afrika.
Mashabiki
wangu nataka niwaambie kwamba nitajitahidi kuboresha kazi zangu na
natamani Talk Show bora East and Central Africa itoke Tanzania.
MO BLOG: Ni nchi zipi ambazo ‘Ongea na Janet’ inaonekana Afrika..?
JANET:
‘Ongea na Janet ‘ inaonekana hapa nyumbani Tanzania, Uganda, Kenya,
Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
(DRC), hivyo naweza kusema ‘Ongea na Janet’ bado ina kazi kubwa ya
kufanya si kwa ajili yangu bali kwa ajili ya watanzania wote.
MO BLOG: Baada ya kuingia mkataba na Dstv nini kilifuata..?
JANET: Baada
ya kuingia mkataba nao fanikio la kwanza ilikuwa ni kubadilisha ‘set
up’ ya kipindi kama nilivyosema na fanikio lingine ambalo lilikuwa ni
ndoto yangu ya siku nyingi ni kuanzisha kampuni yangu mwenyewe ambayo
itafanya vitu ambavyo natamani kuvifanya na tayari nimeshaifungua.
‘Soon’
itaanza ku-produce yenyewe kipindi cha ‘Ongea na Janet’, lakini sasa
hivi tuko kwenye production ya kipindi kingine ambacho ni product ya
‘Ongea na Janet’ kwa hiyo watanzania wakae katika mkao wa kula kwani
nitawaletea vipindi vingine viwili japo sita tangaza mimi.
Kwa sasa
hivi kampuni yangu inafanya ‘production’ kwa hiyo nimekuwa na Media
House, kwa mfano ukija na movie yako tunakurekodia, ukiwa na series zako
tunakurekodia, dokumentari yako tunakutengenezea.
Kitu kingine namshukuru Mungu Dstv wamezidi kunifungulia milango kwani wamenifanya kuwa ‘agent’
wao kwa hapa nyumbani Tanzania. Kwa hiyo nimekuwa katikati ya mpishi na
mlaji upande wa filamu, series na vipindi kwa hiyo kama kuna mtu sasa
hivi ana kipindi anataka kiende Dstv anakileta kwangu, sisi tunakihariri
upya, tunakifanyia ‘sub title’ kisha tunakipeleka Dstv.
Ilimradi hiyo kazi iwe ni ya kwake mwenyewe na ameisajili COSOTA.
Janet Sosthenes Mwenda akiwa katika mahojiano na mgeni.
MO BLOG: Uwakala wa kusambaza movies hapa nchini ulikuwa na ukifanywa na watu waliokutangulia vipi kuhusu ushindani..?
JANET: Ushindani
ni mkubwa haswa kwa mtu wa kati, kwangu mimi changamoto kubwa ni kwamba
bado ni mpya, halafu watu hawajazoea kufanya kazi na mimi kwa hivyo
hawajui. Isipokuwa sisi kiukweli kampuni tumejipanga vizuri kiutawala,
kwa sababu kampuni ina wajumbe wa bodi, ina General Manager, ina
Admnistrator kwa kifupi wafanyakazi sasa hivi wako 10.
Kingine
tunacho kifanya katika kampuni yetu ni kwenda na muda, ukileta kazi yako
then unakotaka iende waki confirm sisi tunapeleka ile zungusha zungusha
sisi hapana. Na kama kazi yako iko chini ya kiwango tumakwambia ukweli
kwa sababu watu wanafeli kwenye ubora wa picha na sauti.
Janet Sosthenes Mwenda akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kipindi chake.
MO BLOG: Kama Janet Sosteneth Mwenda Ongea na Janet imekubadilisha lolote..?
JANET: Kwa kweli ‘Ongea na Janet’ imenipa ‘peace of mind’
kwa sababu ni kitu nilichokuwa natamani kukifanya miaka mingi sana
lakini sikuwa nikipata upenyo na kwa kweli naomba nichukue nafasi hii
kuwashukuru ‘CLOUDS’ kwa sababu wamenipa ‘room’ nzuri
sana yaani pale ni nyumbani kwangu, kwa maana ya kwamba ninapowahitaji
wao tayari wapo kwa ajili yangu.
Na kuanzia
hapo ndio changamoto zikaanza kuonekana, na nadhani kwa wakati ule
nilikuwa mtu wa kwanza kutoka nje na kipindi, lakini sasa hivi vinaingia
vingi na vitakuja vingi kwa kuwa tunaingia katika ‘Digitali’.
Naushukuru sana uongozi wa CLOUDS kwa kunisaidia na wafanyakazi kwa kunipa ushirikiano.
Lakini tena
sana niwashukuru wananchi wanaongalia ‘Ongea na Janet’ kupitia kipindi
hiki nimegundua kuwa watu wengi walikuwa na mambo mengi ya kuzungumza
ila hawakuwana pa kuzungumzia.
MO BLOG: Kipindi cha ‘Ongea na Janet’ kinarushwa hewani saa ngapi na katika televisheni zipi..?
JANET: Kwa
mara ya kwanza kilikuwa kikirushwa hewani saa tatu kamili kila Alhamisi
na Clouds TV na kurudiwa siku ya Ijumaa saa nane mchana na Jumapili saa
kumi na moja jioni.
Lakini niliporudi ‘Season Two’
ambayo ni kibiashara zaidi, nikaongeza sasa inaonekana Jumanne Saa Tatu
na Nusu Usiku hadi Saa Nne na Robo na Alhamisi Saa Tatu usiku na
marudio yapo.
MO BLOG: Vipi katika ratiba ya kipindi hicho kurushwa Dstv..?
JANET: Dstv ni Chaneli 158 SWAHILI AFRICA MAGIC
wanaonyesha pia Jumanne na Alhamisi kama ilivyo hapa Dar es Salaam na
muda ni ule ule, ujanua nina mkataba mrefu kidogo na Dstv na pia
sitegemei kuondoka CLOUDS.
MO BLOG: Unalipi la kuwaambia watanzania lolote lile sio la fani yako.
JANET: Kinachoniumiza
naona kama amani inataka kupotea nchini mwangu hivyo mimi naomba tu
wanaohusika watusaidie, kwa sababu ukitaka kujua ubaya wa kutokuwa na
amani, anzia nyumbani kwako usipokuwa na amani na mtu unayeishi naye
nyumba haikali au siyo.? Hivi sisi kweli leo tukawe wageni kwa watu? Hii
kitu kidogo inaniumiza.
MO BLOG: Nikurejeshe hapohapo kama “Ongea na Janet’ kwa nini ukafikia kuongea maneno hayo..?
JANET: Kwa
sababu ukifuatilia sana kipindi changu vitu vingi ambavyo naongea ni
kujaribu kutoa elimu kutokana na ama matatizo tunayokutana nayo,
kujifunza kutokana na vitu ambavyo vinatukwaza kwenye maisha na kuwekana
sawa.
Hata siku
moja huwezi kuona nazungumzia uchochezi wa kitu Fulani, kipindi changu
ni cha amani na namuomba Mwenyezi Mungu anisaidie angalau niwe mmoja wa
waleta amani nchini kwa kinywa changu, kwa sababu kuna wengine wanaleta
amani kwa peni si ndio? Lakini mimi kwa kinywa changu niweze kuleta
amani.
Kwa hiyo
namuomba mtu yeyote ajifikirie kabla hajafanya chochote, hata kama
umekasirika kiasi gani, jiulize nikishafanya hivi faida yake nini? Hata
huyo unayemuumiza, ukimuumiza unafaidika nini. Kwa hivyo kila mtu
ampende na amheshimu mwingine kwa imani yake.
Wakati
naiombea nchi yangu amani, naomba watanzania wajue kwamba vijana
tumeamua kufanya kazi watupe support: naomba pia nichukue nafasi hii kwa
vijana wenzangu ambao hawapendi kazi, hakuna njia ya mkato kwenye
maisha.
Rais wangu alisema ‘MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA’ na mimi naongeza la kwangu ‘BILA KUFANYA KAZI HAKUNA MAISHA BORA’.
MO BLOG: Janet
Sosthenes Mwenda Mo Blog tunakushukuru kwa kuzungumza nasi machache
kuhusiana na maendeleo ya kipindi chako na pia kukupongeza kwa kuweza
kufikia hapo ulipofikia na kukutaka usikate tamaa pambana utafika.
JANET: Akhsante
sana ndugu zangu wa Mo Blog nanyi nawashukuru sana kwa kunithamini na
kutaka kujua nimefikia wapi kwa faida ya watanzania. Na nawaambia
watanzania hasa vijana wawe wanatembelea mtandao wa www.dewjiblog.com watapata habari nyingi za kuelimisha, kufurahisha, burudani , michezo na pia kuangalia nafasi za kazi zinapotolewa.
MO BLOG: Waambie watambue !! Ciao..!!
JANET: Ok Bye.!
No comments :
Post a Comment