Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa naodha wa timu ya Business Times Queens, Lulu Habibu baada ya kuifunga TBC 39-18 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe
la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa naodha wa timu ya Jambo Leo, Said
Mwishehe katika baada ya kuifunga Changamoto bao 1-0 katika mchezo wa fainali
uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akimkabidhi kombe la Ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 kwa naodha wa timu ya Business Times Queens, Lulu Habibu baada ya kuifunga TBC 39-18 katika mchezo wa fainali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
Naibu
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akikagua
timu ya Business Times Queens kabla ya mchezo wao dhidi ya TBC.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akikagua kikosi cha timu ya TBC Queens.
Kikosi cha TBC Queens kikiwa katika picha ya pamoja.
Mabingwa wa
Netiboli wa Kombe la NSSF Media Cup 2013 Business Times Queens kikiwa
katika picha ya pamoja kabla ya kuumana na TBC katika fainali.
Mabingwa wa
soka wa michuano ya NSSF Media Cup 2013 Jambo Leo, katika picha ya
pamoja kabla ya mechi ya fainali dhidi ya Changamoto.
Kikosi cha timu ya Changamoto kilichoshika nafasi ya pili NSSF Media Cup 2013
Beki wa
Changamoto John Robert akichuana na mshambuliaji wa Jambo Leo, Rogatius
Katyali katika mchezo wa fainali ya michuano ya NSSF Media Cup 2013.
Wachezaji wa Jambo Leo wakifurahia ushindi wa timu yao.
Mashabiki wa timu ya Netiboli ya Business Times wakishangilia ushindi wa timu yao.
Naibu Waziri
wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makala akizungumza katika
hafla ya kufunga michuano ya NSSF Media Cup 2013 leo.
DAR ES SALAAM, Tanzania
TIMU za Jambo Leo na Business Times (BTL), leo zimefanikiwa
kutwaa ubingwa wa michuano ya NSSF Media Cup 2013, baada ya kushinda mechi zao
za fainali ya soka na netiboli dhidi ya Changamoto na TBC.
Katika fainali ya soka, bao pekee la kipindi cha kwanza la
mshambuliaji Julius Kihampa, lilitosha kuwapa Jambo Leo ubingwa wa pili wa
michuano hiyo iliyofanyika kwa mwaka wa 10 na harakati za Changamoto
kusawazisha hazikuzaa matunda.
Kwa upande wa Netiboli, Business Times Queens ‘The Bize,’
ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mchezo huo kwa ushindi wa magoli 39-18 dhidi ya
TBC, huku nyota wake Lulu Habibu akifunga mara 27.
Lulu alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo upande
wa netiboli kwa kufikisha magoli 153 katika mechi nne alizocheza, huku tuzo
hiyo kwa upande wa soka ikitwaliwa na Nurdin Msindo wa Tumaini Media,
aliyefunga mabao manne.
Lulu na Nurdin kila mmoja alizawadiwa kiasi cha shilingi
300,000 ambayo ni zawadi kwa wafungaji bora, huku Sahara Media ikitwaa tuzo ya
timu yenye nidhamu, ambapo walizawadiwa kikombe.
Kwa kutwaa ubingwa soka, Jambo Leo walizawadiwa kikombe na
shilingi mil. 4, huku Changamoto wakitwaa shilingi mil. 3 kwa kushika nafasi ya
pili na TBC wakizoa shilingi mil. 2 kwa kutwaa nafasi ya tatu - baada ya juzi
Ijumaa kuwalaza IPP kwa penati 4-3.
‘The Bize Queens’, wamebeba kombe na shilingi mil. 3.5 za ubingwa
wa netiboli, huku mshindi wa pili TBC wakilamba shilingi mil. 2 na mshindi wa
tatu NSSF wakibeba kombe pekee na kitita chao cha shilingi mil. 1 wakikitoa kwa
Tumaini iliyoshika nafasi ya nne.
NSSF Media Cup 2013 ni michuano iliyofanyika kwa wiki mbili
kwenye viwanja vya TCC na DUCE vilivyoko Chang’ombe jijini Dar es Salaam,
ikihusisha timu 17 za soka na 15 za netiboli zilizoundwa na wafanyakazi wa
vyombo vya habari nchini.
Baada ya michuano hiyo kuzinduliwa na Waziri wa Kazi na
Ajira, Gaundencia Kabaka Machi 9, ilihitimishwa leo kwa Naibu Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla kukabidhi zawadi kwa washindi
wapya.
No comments :
Post a Comment