Msijitutumue na kuwakoga mliowashinda kwenye uchaguzi.
Sasa kazi muhimu ya UVCCM ni moja tu, kuifanya CCM ishinde chaguzi zote.
NA BASHIR NKOROMO.
MOROGOROMWENYEKITI
wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Hamis Juma Sadifa amesema
baada ya uchaguzi mkuu wa Jumuia hiyo uliomalizika mwishoni mwa mwaka
jana, sasa kazi iliyopo mbele ya UVCCM ni kuhakikisha CCM ni inaimarika
zaidi na kushinda chaguzi zote.
Amesema
baada ya uchaguzi huo na uteuzi wa Viongozi wa Baraza Kuu, wajibu
walionao viongozi wa Jumuia hiyo sasa ni kujishusha chini na kuacha
kabisa tabia ya kujitutumua na kuwagoga waliowashinda kwenye uchaguzi
ikiwa ni njia mojawapo ya kuvunja makundi ndani ya jumuia hiyo.
Sadifa
alisema hayo, Februari 28, mwaka huu, wakati akizungumza na Baraza Kuu
la UVCCM mkoa wa Morogoro, alipowasili kwa ajili ya ziara ya siku tatu
mkoani humo ambayo ni ya kwanza kufanya nchini tangu kuchaguliwa kwake
kuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyo.
"Baada
ya uchaguzi kumalizika na kukamilisha uteuzi wa wajumbe wa Baraza letu
kuu, sasa kazi iliyobaki mbele ya ni kuhakikisha CCM inakuwa imara na
kushinda chaguzi zote zinazokuja. Wale tuliochaguliwa sasa tujishushe
kwa wanachama wetu, na kuacha kabisa tabia tuliyonayo baadhi yetu ya
kujitutumua na kuwakoga tuliowashinda, tabia hizo hazina faida na ni
sumu kabisa kwa uhai wa Jumuia na Chama chetu", alisema.
"Tabia
hiii tuiache kabisa, ni sumu inayoendeleza makundi yaliyotokana na
uchaguzi, kuendelea kwake ndiko kumekuwa kukisababisha CCM kushindwa
katika chaguzi mbalimbali hata katika maeneo ambayo wapinzani wala
hawajai mkononi, eeh, wakipata kura zao kidogo na za sisi wenyewe
tunaovurugana wanashinda!" alisema.
Alisema,
ni wajibu wa viongozi walipata nyadhifa, kuwabembeleza waliowashinda
ili kuwaleta karuibu yao, badala ya kuwananga na hivyo kusababisha
kujenga mpasuko ndani ya Jumuia hiyo ambao alisema siyo lazima kuwepo
kama busara hiyo inatumika.
"Wewe
ukishakuwa kiongozi, jitahishi kutumia kila mbinu kuhakikisha yule
uliyemshinda au ambaye hakukuunga mkono wakati unatafuta ushindi unakuwa
karibu naye kiasi cha kujenga urafiki wa kumfanya akuamini kwamba wewe
ni muungwana, hivyo ndivyo siasa inavyotakiwa kufanywa", alisema Sadifa
na kuongeza;
"Unajaribu
kwa mara ya kwanza kumvuta, ukishindwa unajaribu tena hata mara ya pili
hadi ya tatu, kama naye ni muungwana lazima ataondoa kinyongo, na kama
ukiona haelekei kuwa kuondoa kinyongo mwache, lakini usimchukie kabisa
maana kama hakukuunga mkono wakati huu ipo siku atakuunga mkono kwa
jambo jingine".
Katika
ziara hiyo, Mwenyekiti huyo wa UVCCM, yupo pamoja na viongozi wengine
wa Kitaifa wa Jumuia hiyo wakiwemo Katibu Mkuu, Martine Shigella na
Naibu Katibu Mkuu Mfaume Kizigo na makada wawili wa aliohamia CCM hivi
karibuni wakitoka Chadema, Mwampamba na
Katika
siku tatu za ziara hiyo viongozi hao watatakwanyika wilaya karibu zote
za mkoa wa Morogoro na kushambulia kila kona kuimarisha uhai wa Chama.
No comments :
Post a Comment