Bondia
mwenye makeke mengi na asiyekubali kushindwa ulingoni na , Cosmas
Kibuga, anatarajia kupanda ulingoni siku ya jumapili wiki hii katika
ukumbi wa Texas Manzese, kuzipiga na bondia mkongwe, Sweet Kalulu,
katika pambano la kirafiki la kusherehekea Pasaka.
Akilizungumzia pambano hilo muandaaji wa mchezo huo, Miraji
Msusa, alisema “burudani yetu ni kuangalia ngumi na kushangilia na
najua ngumi nzuri zipo katika hawa mabondia wasio na majina na wenye
upinzani mkali ,nikaonelea lazima katika sikukuu hii ya pasaka tusiiache
ipite hivihivi bila kupata starehe yetu, kusubiri mpaka tarehe 7 april kwenye pambano kubwa la pale ccm mwinjuma-mwanayamala ni mbali, Nikaafikiana na cosmas kibuga na sweet kalulu ambao ni wapinzani mitaani wamalizie kiu yao hiyo''. alisema
No comments :
Post a Comment