Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, March 20, 2013

AZAM FC walakiwa KWA SHANGWE JIJINI DAR


Pichani ni baadhi ya wachezaji hao walipowasili uwanjani hapo.
Baadhi ya mashabiki na wapenzi wa timu ya Azam FC wakicheza ngoma kwa furaha wakati wa mapokezi ya timu hiyo leo asubuhi.
SIMBA, YANGA ZILILIPENDWA... hivi ndivyo shabiki huyu wa Azam FC alivyoandika jezi yake na akitoa salamu kwa Watani hao wa jadi katika soka nchini.
Wachezaji wa Azam FC wakipanda basi lao

Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog

Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, AZAM FC, wamerejea jijini Dar es Salaam leo asubuhi  na kupokelewa kwa shangwe na mashabiki na wapenzi wa timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Azam waliwasili kwa mafungu kwa ndege ya Kenya Airways ambapo baadhi ya wachezaji wakiwapo wanaoichezea Taifa Stars kubaki Nairobi isipokuwa Mcha.

Azam ambao msimu huu wapo nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Tanzania bara walikuwa Nchini Liberia kuchuana na timu ya Barrack Young Controllers (BYC) ambapo Azam walishinda 2-1 katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman Monrovia, Liberia.

Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.

No comments :

Post a Comment