Mshindi wa Miss Utalii Vipaji kutoka Mkoa wa Manyara wa (katikati) akiwa na washindi wenzake wawili waliofika mpaka Tatu bora
Na Mwandishi Wetu
Hatimaye
Mshiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kupitia mkoa wa Manyara wake
imeshinda tuzo la vipaji 2012/13 na kuibwaga mikoa mengine wa mikoa 29
ya tanzania bara na zanzibar Mary 19 alionesha vipaji vya hali ya juu
katika ushindani ambao
ulikuwa mkubwa hasa kutoka kwa warembo wa mikoa ya Lindi , Kagera, Dodoma, Zanzibar, Katavi, hata hivyo
mchuano
ulikuwa mkali zaidi kati ya Miss Utalii, Lindi Manyara na Kagera ambao
walionesha Umahili mkubwa wa kucheza ngoma za asili na kupelekea kuingia
katika hatua ya Tatu Bora.
Katika Hatua
hiyo ya Tatu Bora washirika hao walicheza wimbo mmoja ujulikanao kwa
jina la katope kutoka kundi la ngoma za asili la kibiriti ambao ni
mchanganyiko wa ngoma mbalimbali wa makabila ya ngoma za kusini.
Katika Hali
iliyo wafanya wapenzi wa Fani ya Urembo waliofulika katika ukumbi wa Dar
Live Mbagala kuto kuamini kwamba wanao cheza jukwaani ni Mabinti wa
Kizazi kipya ambao kwa Hali ya kawaida ya sasa ni nadra sana kumuona
sister Duu tena Mrembo kucheza ngoma za asili kwa ufasaha na umahili
mkubwa.
Hivyo
kuwafanya wapenzi hao kuacha viti vyao na kuanza kushangilia kwa nguvu
mwanzo hadi mwisho huku wakiwapongeza waandaaji wa shindano la Miss
Utalii Tanzania kuwa ni Hazina kubwa ya utamaduni wa Mtanzania na
Wengine wakithubutu kusema Miss Utalii ni mtambo wa kurekebisha tabia
kwa kuweza kuwabadirisha fikra za mabinti hao wa kizazi kupya
mashindano hayo kwa ya kuwa kucheza ngoma za asili ni ushamba hadi
kuwafanya kuwa wacheza ngoma mahili tena hadhalani bila ya aibu na kwa
kujivunia utamaduni na Ngoma za Asili Tanzania. Wengi wa wapenzi
waliohudhulia katika
shindano hilo
wakisika kwa nyakati tofauti kuitaka na kuishauli serikali na mamlaka za
utalii kudhamini shindano la Miss Utalii Tanzania kwa Faida ya Jamii
na Taifa kwani shindano hili limedhihilisha uwezo mkubwa wa sio tuuu
kuhifadhi utamaduni wa mtanzania bali pia kuhamasisha na kutangaza
utalii wa tanzania kitaifa na kimataifa.
Alisikika
Mpenzi Mmoja aliye julikana kwa jina La Jafary Shaibu akisema kuwa
shindano hili ni zuri na ni lakipekee lakini tatizo inaonekana waandaaji
hawajapata wadhamini wa uhakika, kwanini Serikali isiwasaidie hawa?
Akizungumza
katika Shindano hilo ambalo Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao
alikonga nyoyo za watu kwa Muziki wake wenye asili ya kitanzania, Mgeni
Rasmi Muheshimiwa Maabad Suleiman Hoja Mustahiki Meya wa Manispaa ya
Temeke aliwapongeza sana washiriki na washindi lakini alitoa shukurani
za pekee kwa waandaaji wa mashindano haya kwa kuipa manispaa na wilaya
ya Temeke Heshima kubwa ya kuwa wenyeji wa Tukio hili la kitaifa lenye
hadhi ya kimataifa.
Alisema
kwamba hii ni heshima kubwa kwa Manispaa ya Temeke wilaya ya Temeke
Tunao uwezo na Hadhi kuwa wenyeji wa matukio makubwa ya kimataifa na
kitaifa kama hili la miss utalii tanzania 2012/13.
Hivyo kutoa
fulsa ya pekee kwa Temeke kujitangaza kitlii, kitamadunina kiuwekezaji
ndani na nje ya Nchi, aliahidi kuwa manispaa ya Yemeke inatawaunga
mkono kwa Hali na Mali ili kufanikisha fainali hizo ambazo zitafikia
kilele katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Dar es salaam pia aliwataka
wadau mbalimbai kujitokeza kudhamini shindano hilo.
Mshindi wa
Tuzo hiyo ya Vipaji ambaye alishangiliwa na washiriki wote baada ya
kutangazwa kama mshindi, alizawadia Scholarship ya kusoma kozi ya
Kiwango cha Diploma katika chuo chochote nchini.
Fainali za
Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering
Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General
Suppries Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland
Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata
Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA
No comments :
Post a Comment