KAMPUNI ya QS Mhonda J Entertainment imeandaa
tamasha la muziki wa Injili liitwalo, Tumaini Jipya Gospel Concert, ambalo
litafanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro, Machi 31 mwaka 2013 ambayo
itakuwa Siku Kuu ya Pasaka.
Dhumini kubwa la kuandaa tamasha hili ni kutaka
kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum kwenye jamii ikiwemo watoto yatima pamoja
na wale wanaishi katika mazingira magumu, kutoa misaada kwenye hospitali pamoja
na Makanisa yaliyopo mjini Morogoro.
Tumaini Jipya Gospel Concert limeanzia Morogoro
lakini litaendelea kwenye mikoa mingine ya Tanzania Bara, kwa kipindi chote cha
mwaka huu wa 2013 likiwa na lengo lile lile la kutoa tumaini kwa jamii.
Katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania
litapambwa na Waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni
Bahati Bukuku, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara
Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.
Mbali na waimbaji hao lakini zitakuwepo kwaya na
vikundi mbalimbali vya muziki wa Injili Tanzania ikiwemo, Rafiki Gospel
Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC huku Masanja Makandamizaji
akipewa jukumu la kuongoza shughuli hiyo (MC).
Sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia
waimbaji tuliowataja lakini tutakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya
Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi.
Aidha katika tamasha la Tumaini Jipya tunatarajia
kuwaweka pamoja watu zaidi ya elfu 30 kutoka katika viunga vyote vya mji wa
Morogoro kwa lengo la kuwapa tumaini jipya.
Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa
Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku kuu
ya Pasaka kwa kufika kwao katika tamasha la Tumaini jipya ili kupata tumaini
jipya.
Imeandaliwa na:-
QS Joseph
Mhonda-Mkurugenzi Mtendaji wa QS Mhonda J Entertainment.
No comments :
Post a Comment