Mgeni rasmi katika
mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2013, Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara
akiwahutubia washiriki na wakazi wa mjini wa moshi muda mfupi baada ya
kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbizo hizo kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika
Moshi. (MUCCoBS). (Picha na Dixon Busagaga)
Baadhi ya washiriki wa mbio kujifurahisha
‘Vodacom 5 Km Fun Run,’ wakishiriki katika mbio hizo ambazo ni sehemu ya
Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013. (Na Mpiga Picha Wetu)
Kocha
Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen, akimaliza mbio za
Kilimanjaro Premium Lager Half Marathon, zilizofanyika jana mjini
Moshi.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka
akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kwa wanawake, Zakia Mrisho katika mbio za
Vodacom 5 KM, za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2013, mjini Moshi. (Picha na Dixon
Busagaga)
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,
George Kavishe, akimpongeza mshindi wa mbio za kilomita 21, Sarah Ramadhani, kwa
wanwake, katika mashindano ya Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zilizofanyika
mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Wakimbiaji wa Kenya
wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio hizo.
Mfukuza
Upepo kutoka Nchini Kenya na Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika Mbio za
Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo
wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Eunice Muchiri akikimbia na
kumaliza wapili mbio za Kilimeta 42 Wanawake, katika Mbio za Kilimanjaro
Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha
Ushirika Mjini Moshi.
Hakika mbio si kitu lelema,
hapa ni Eunice Muchiri akitaapika baada ya kumaliza mbio hizo.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio
za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na kuwa
kocha wa Kwanza wa Timu ya Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa kwake
miaka 10 iliyopita.
Kocha Mkuu
wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akisalimia mashabiki
waliokuwa wakimshangilia baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio za
nyika za Kilimanjaro 2013. (Picha na Father Kidevu
Blog)
No comments :
Post a Comment