Pambano la masumbwi kutetea makanda
wa mabara wa WBF(world boxing forum) wategemea kufanyika katika uwanja wa
mkwakwani jijini Tanga kwa kuwakutanisha Alan
Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa mkanda
huo aliouchukua nchini Malawi kwa
kuzipiga na Jumanne Mohamed wa tanga
ambae anavyo vigezo na sifa
zote za kuugombania ubingwa huo.
Jumanne Mohamed ambae alipata
nafasi ya kugombania ubingwa
wa dunia nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na
mnamibia nafasi hiyo imejirudia
tena,safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini
mwake.
Muandaaji wa pambano hilo Ally
Mwanzoa akizungumza na viongozi wa ngumi nchini pamoja na katibu
mkuu wa ngumi za kulipwa Ibrahim kamwe
amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan kamote autetee mkanda wake alioupata Blantaya nchini Malawi usije ukapoteza kwa
kutokuutetea ubingwa wake huo, na kukaa na uongozi wa ngumi kwa kuangalia bondia gani anafaa
na ikaamuliwa jumanne Mohamed
anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko
mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi.mwanzoa
aliendelea kwa kusema pia kutakuwa na
mapambano mengine ya utangulizi kati jj
ngotiko na haji juma wa Tanga katika pambano la raund
kumi, na kutakuwepo na mapambno mengine mengi y a utangulizi.
No comments :
Post a Comment