Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, March 11, 2013

Bingwa wa dunia mchezo wa Kareti kutengeneza filamu inayopinga mauaji ya walemavu wa ngozi




Mwandishi Wetu


KAMPUNI ya  Advanced security Limited imeingia  makubaliano na bingwa wa dunia wa mchezo wa Kareti, Profesa Maurizio Martina wa Italia kwa ajili ya kutengeneza filamu mbalimbali pamoja na ile inayopinga mauaji ya walemavu wa ngozi, albino na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Makubaliano hayo yalifanyika jana kwenye hotel ya JB Delmonte na filamu hiyo itaanza kurekodiwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na kukamilika kwa miezi mitatu.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile alisema kuwa  sababu kubwa ya kuingia katika masuala ya filamu ni moja ya shughuli zake katika kujihusisha na masuala ya jamii.
Ndambile alisema kuwa kampuni yao ni Limited na kutokana na hilo inaweza kufanya shughuli nyingine mbalimbali tofauti na huduma ya ulinzi na usalama.
Alisema kuwa katika filamu hiyo, atawashirikisha waigizaji mbali mbali wa hapa nyumbani na wapo mbioni kukamilisha taratibu zote kwa mujibu wa sheria ya kurekodi filamu hapa nchini.
Kwa mujibu wa Ndambile, Profesa  Maurizio  ambaye ameigiza filamu nyingi katika nchi za mbali mbali pamoja na Uingereza na Marekani mbali ya Italia atashirikiana na mke wake, Angel Howel na mwanaye, Dumiano ambaye amewahi kuigiza na mcheza filamu maarufu duniani.
Profesa Maurizio alisema kuwa pia atafundisha wanawake jinsi ya kujilinda kwa kutumia mchezo wa karate ili kuondoa unyanyasaji wa wanawake nchini.
Amesema kuwa amefanya kazi  hiyo nchi mbali mbali ikiwa pamoja na DR Congo na Afrika Kusini.
“Lengo la filamu yangu ni kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mila potofu za kuwaangamiza albino na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake,” alisema Profesa Maurizio ambaye pia ni Rais wa Dunia wa Shirikisho la Mchezo wa Kareti.

No comments :

Post a Comment