Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Rubelyn Alcantara akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisini mwa Push Observer, Kinondoni.
Baadhi
ya maofisa kutoka makampuni mbali mbali wakielekezwa jinsi kampuni ya
Push Observer inavyofanya shughuli zake kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi
wa kampuni hiyo.
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
za mitandao ya simu za mikononi nchini zimeshika nafasi ya
kwanza katika kutangaza biashara zao kwenye vya habari nchini kwa robo
ya mwisho ya mwaka jana.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni inayoongoza katika kusimamia
na kufuatilia mwenendo wa vyombo vya habari nchini, Push Observer,
kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel ndiyo inayoshika nafasi ya kwanza
kwa kutangaza matangazo mengi nchini.
Mkurugenzi
mtendaji wa Push Observer, Ruby Alcantara alisema kuwa kampuni ya pili
ni Tigo na kufuatiwa na Vodacom Tanzani katika nafasi ya tatu na Zantel
katika nafasi ya nne. Kampuni ya bia Tanzania (TBL) inashika nafasi ya
tano ikifuatiwa na Pepsi, Star Times, Coca Cola, SBL na Twaweza katika
nafasi ya 10.
Bi.
Alcantara alisema kuwa takwimu hizo ni za uhakika kutokana na kukusanya
rekodi hizo kwa kupitia vifaa vya kisasa walivyowekeza katika sekta
hiyo.
Alisema
kuwa jumla ya fedha zilizotumika kwa makampuni yote 20 bora katika
kutangaza biashara ni sh bilioni 17, 827,970, ingawa taarifa hiyo haija
ainisha gharama halisi ya kila kampuni ilizotumia katika kutangaza
bidhaa zake.
“
Hatuwezi kuweka bayani ni kiasi gani cha fedha kimetumika katika zoezi
hili, ni vigumu kufanya hivyo, lakini takwimu zetu ni sahihi kutokana na
vifaa tulivyowekeza katika kutoa huduma hii, ni ya kisasa na yenye
ubora wa kimataifa, tutakuwa tunatoa taaifa hizi kila baada ya miezi
mine,” alisema.
Alisema
kuwa vyombo vya habari vinavyofaidika kwa kupata matangazo mengi ni
redio na televisheni. Amesema kuwa kampuni yao itakuwa inatoa taarifa
kuhusiana na watangazaji bora wa kwenye vyombo vya habari kila baada ya
miezi mitatu. Ripoti robo ya kwanza ya mwaka huu inatarajiwa kutolewa
mwezi ujao mwanzoni.
“Ripoti
hii inatoa fursa kwa kila kampuni kujua utendaji wake katika ushindani
wa kibiashara, pia kujua mshindani wako anafanya nini katika
kujitangaza na kukuwezesha kubadili mbinu ili uweze kuendeleza
ushindani au kuweza kuendelea kushika nafasi ya kwanza kibiashara,”
alisema.
No comments :
Post a Comment