Katibu Mkuu, BFT, Makore Mashaga |
MASHINDANO ya Taifa kwa mchezo wa ngumi za ridhaa
yanatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi ujao baada ya kufanyika kwa mashindano ya
ngazi za chini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu
wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Mashaga Makore, alisema kuwa
washindi watakaopatikana katika ngazi za chini ndiyo watakaoingia kwenye
mashindano ya Taifa.
Amesema kuwa kwa sasa mashindano hayo yataanza
katika ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa baada ya hapo washindi watashiriki
mashindano ya Kanda ambapo Kanda nne zimetengwa kwa ajili ya mashindano hayo
kabla ya Taifa.
“Mwaka huu tumefanya tofauti na miaka iliyopita
ambapo sasa tumeanzia ngazi za chini ili kuwapata mwachezaji ambao
wataliwakilisha taifa kwenye michuano mbalimbali.
“Kabla hatujaanza mashindano ya Taifa kutakuwepo na
mashindano ya Kanda ambayo yatashirikisha mabondia au timu zilizofanya vizuri
ngazi ya Kata, Wilaya na Mikoa, hao ndiyo watakuwa na sifa ya kushiriki ngazi
ya Taifa,” almesema Makore.
Almesema katika Kalenda ya BFT ya mwaka huu, kuna
mabadiriko mbalimbali ambayo yanamtaka kila mjumbe wa Kamati ya Utendaji
kuwajibika kulingana na majukumu aliyopewa.
“Mwanzo shughuli zote zilikuwa zinafanywa na uongozi
wa BFT wakati kuna kamati zake, lakini hivi kuna tofauti katika Kalenda ambapo
kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa maagizo ya kamati yake
inavyomtaka afanye ili kukuza na kuendeleza mchezo huu,” amesema Makore.
No comments :
Post a Comment