SHULE
ya Sekondari Majani ya Chai iliyoko wilayani Ilala, Dar es Salaam inakabiliwa na tatizo la baadhi
ya wanafunzi wanaojiunga kutokujua kusoma kwa ufasaha.
Kauli
hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam leo na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Jasinta Assey, alipozungumza na waandishi
wa habari kuhusu malalamiko yaliyotolewa na wazazi kuwa baadhi ya walimu wa
shule hiyo hawafundishi ipasavyo, kitendo ambacho si kweli.
Alisema
mfano mzuri ni matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka jana ambapo wanafunzi
76 kati 276 walikuwa hawajui kusoma, kitendo kilichoongeza idadi ya wanafunzi
waliofeli katika shule hiyo.
“Walimu
wa sekondari tuna kazi kubwa, kwani tunawapokea watoto ambao wengi wao wana
matatizo ya kutojua kusoma na matokeo yake ni kushindwa kabisa kuzingatia
masomo wawapo shuleni,” alisema.
Assey
alisema licha ya hilo, shule hivi sasa inakabiliwa na tatizo
la baadhi ya wanafunzi wa kike na kiume kujiingiza kwenye vitendo vya utumiaji
wa mihadarati hususan bangi ambayo imekuwa ikiuzwa na baadhi wakazi
wanaoizunguka shule hiyo.
Alisema
mfano mzuri ni juzi Jumanne,
wanafunzi 49 kati ya 54 wa kidato
cha nne wanaosoma masomo ya sanaa walipotoroka darasani na kukutwa kwenye
makundi ya wavuta bangi na kwamba hivi
karibuni mkazi mmoja aliokota nguo za mmoja wa wanafunzi alizokuwa
amenyang’anywa na kutupwa vichakani.
No comments :
Post a Comment