Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lilianza mwaka 2004 katika ukumbi wa
Traventine, mwaka 2008 lilifanyika Msasani club, mwaka 2009 likafanyika
P.T.A. Hall iliyoko ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere Kilwa
road, mwaka 2010 likafanyika Diamond Jubilee Hall na mwaka 2011 likafanyika
tena P.T.A. Hall.
Mwaka huu 2012, tamasha la Mitikisiko ya Pwani linafanyika ukumbi
wa Dar Live tarehe 3/11/2012 siku ya Jumamosi. Tamasha litafungua milango
saa nne asubuhi. Awamu hii itakuwa ni kwa watoto na watu wazima ambao
ambao wako mbali na jiji au wale ambao hawana rukhsa kutembea usiku.
Na kiingilio kwa awamu hii ni shilingi 5,000/= kwa wakubwa
na watoto shilingi 3,000/=, watapata burudani kutoka katika kundi
maarufu la Wanne Star.
Awamu ya pili itaanza saa mbili usiku hadi majogoo kwa kiingilio cha
shilingi 10,000 tu. Awamu hii itapata burudani kutoka kwa bendi zipatazo
13 za taarab ambazo ni Diamond Taarab Kutoka Zanzibar, Manuari, T.Moto,
Zanzibar Njema, New Zanzibar Modern Taarab, Kings Modern, East Africa
Melody, Dar Modern Taarab, Coast Modern Taarab, Five Star Modern Taarab,
Jahazi Modern, Mashauzi Classic na Bibie Khadija Kopa,
WAUTAKAAA! KIAFRIKA ZAIDI….!
No comments :
Post a Comment