Kariakoo ilivyokuwa leo mara baada ya sala ya Ijumaa, maduka yalifungwa
na watu kulikimbia eneo hilo kukwepa mabomu, ya polisi ambao
walizingira misikiti yote ya Kariakoo kwa kuweka ulinzi mkali.
Polisi wakiweka Doria kali kwenye mitaa
ya Kariakoo jijini Dar es Salaam leo wakati wa Sala ya Ijumaa, ambapo
walidhibiti kila msikiti kwa kuweka ulinzi mkali kuhakikisha hakuna
maandamano yanayofanyika. Hata hivyo mabomu kadhaa yalipigwa kwa watu
waliojaribu kutaka kuandamana na kusababisha eneo la Kariakoo kukimbiwa
na watu na maduka kufungwa.
|
Aidha mmoja wa wafanya biashara Ally Saidi alisema serikali bora itangaze tu kama ijumaa ni siku ya mapumziko maana wao hawafanyi biashara kutokana na mabomu kila inapofika siku ya Ijumaa.
"Serikali wangetumia akili kwa kuwaruhusu hawa watu waandamane kisha wakawalinda waone kama ijumaa nyengine wataandamana badala ya kutumia nguvu nyingi na pesa kulinda misikiti halafu hakuna kinachopatikana zaidi ya vurugu. ZAID TEMBELEA http://saidpowa.blogspot.com/
No comments :
Post a Comment