Tuesday, July 31, 2012
MKURUGENZI MWANAHALISI AILALAMIKIA SERIKALI BAADA YA KUFUNGIA GAZETI LAKE
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali halisi , inayo chapisha
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akiongea na Waandishi wa
habari katika Ofisi za Kampuni hiyo juu ya malalamiko yake kwa
serikali kutokana na kufungiwa kwa gazeti lake la Mwana halisi jana
ambapo alilaani vikali uamuzi huo uliochukuliwa na serikali na hivyo
kuitaka serikali kufuta mara moja Tamko lake Kushoto ni Mhariri wa
Gazeti hilo Bw, Jabir Idrissa.
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akiongea na Waandishi wa
habari katika Ofisi za Kampuni hiyo juu ya malalamiko yake kwa
serikali kutokana na kufungiwa kwa gazeti lake la Mwana halisi jana
ambapo alilaani vikali uamuzi huo uliochukuliwa na serikali na hivyo
kuitaka serikali kufuta mara moja Tamko lake Kushoto ni Mhariri wa
Gazeti hilo Bw, Jabir Idrissa.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
![]() |
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kubenea |
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali halisi , inayo chapisha
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akionyesha baadhi ya Magazeti
yaliyolalamikiwa na Serikali.
Gazeti la Mwana Halisi Bw, Saed Kubenea, akionyesha baadhi ya Magazeti
yaliyolalamikiwa na Serikali.
DEWJI AZIPATIA USHAURI TIMU ZA SIMBA, YANGA

MWANACHAMA maarufu wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Azim Dewji amezishauri klabu kubwa za Simba na Yanga nchini kuanza kuutumia mtaji wa wanachama wake kujijenga kiuchumi, na kuepuka kuwa tegemezi.
Dewji, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashatra maarufu nchini, alisema kwamba kila klabu ina zaidi ya wafuasi milioni 15 nchi nzima, lakini ajabu klabu zinaendelea kuwa ombaomba.
“Huu ni mtaji mkubwa sana, lakini utashangaa klabu haina hata asilimia moja (150,000) ya wanachama wa kweli. Kila siku utasikia wanachama 3,000 hadi 6,000. Kiongozi wa klabu anachaguliwa na wanachama wasiofika 2,000?
“Jamani, kwa klabu inayoshabikiwa na mamilioni ya watu inashindwaje kujijenga kiuchumi kwa kuwatumia mashabiki wake waliozagaa kila kona ya nchi? Jiulize, kama angalau hao watu 150,000 tu wakilipa ada ya mwaka ya 12,000 ambayo hata hivyo bado ni ndogo, si wanaweza kuvuna sh
bilioni 1.8 kwa mwaka, hizi si fedha nyingi?
“Kuna haja ya kufanya mapinduzi ya kweli, badala ya kufikiria kuifunga Simba au Yanga na kutwaa ubingwa wa Bara. Timu yenye uchumi imara, ndiyo inayokuwa na jeuri ya kuwa na kikosi imara na hivyo kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Huko ndiko tunakopaswa kwenda,” alisisitiza.
Aidha, Dewji ameipongeza Yanga kwa kufanikiwa kutetea ubingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwishoni mwa wiki, baada ya kuizamisha Azam kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali wa fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Dewji, aliyewahi kuifadhili Simba na kuifikisha fainali za Kombe la CAF mwaka 1993, alisema pamoja na yeye kuwa `Simba Damu’, ana kila sababu za kuimwagia sifa Yanga kwa kuwa imezika haraka matatizo yake na kugeukia kusaka maendeleo.
“Huwezi kuamini kama Yanga iliyopigwa 5-0 na kuibua tafrani nzito Jangwani, ndiyo hii ya leo. Wameikubali hali na kubadilika ndani ya muda mfupi sana. Wana amani na matunda yake yameonekana ingawa walikuwa na kipindi kifupi cha kusuka timu na kurejesha mshikamano ndani ya klabu.
“Naipongeza Yanga na hasa Mwenyekiti wake, Yussuf Manji kwa sababu naamini imani ya wanachama juu yake ndiyo iliyorekebisha hali haraka, naye kama kiongozi kuhakikisha usajili makini unafanyika, kocha anapatikana na uzalendo ndani ya Yanga unarejea,” alisema Dewji.
Aliongeza kuwa, pamoja na matunda ya haraka ya uongozi wa Manji, wana-Yanga wanapaswa kumpa ushirikiano ili kuiondoa Yanga katika utegemezi wa miaka nenda rudi, huku akisisitiza Manji hatabaki Yanga milele.
“Wana kiongozi shupavu, sasa washirikiane naye kuujenga uchumi wa klabu. Haya mambo ya kutegemea mtu kila kukicha si mazuri. Na hili si kwa Yanga tu, hata Simba na klabu nyingine zinapaswa kujikita katika kujijenga kiuchumi ili ziwe na jeuri ya fedha bila ya kutegemea mifuko ya mwanachama mmoja mmoja,” alisema.
MABALOZI WA HARAMBEE YA UJENZI WA HOSTELI ZA WASICHANA WA SEKONDARI WAZINDUA KAMPENI YA ELIMU YAO WAJIBU WETU
Waandishi wa habari waliofika kuhudhuria uzinduzi wa ‘Elimu yao, Wajibu wetu” kampeni iliyoandaliwa na mabalozi waliojitolea kwa hiari kuhakikisha fedha hizo zinapatikana. Kiasi chote kitakachopatikana katika kampeni hiyo kitaingizwa katika mradi huu.
Kikundi cha wasichana
maarufu watano katika nyanja mbalimbali nchini wameungana kwa pamoja na kuamua
kwa hiari kuunga mkono jitihada za Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) za kutafuta
kiasi cha shilingi za kitanzania billion 2.3 zitakazotumika kujenga hosteli 30
ambazo zitahudumia wasichana wa shule za sekondari 1,504.
Kikundi hicho cha mabalozi
wa kampeni hii kinaundwa na Rebeca Gyumi(Mtangazaji wa kipindi cha FEMA) Faraja
Nyalandu (Miss Tanzania 2004), Nancy Sumari (Miss Tanzania 2005) Jokate
Mwegelo(Mshindi wa pili Miss Tanzania 2006) na Mariam Ndaba(Mwana mitindo na
mmiliki wa blog) kiliguswa kwa namna ya kipekee na na jitihada za TEA na hivyo
wakaamua kwa hiari kuungana na TEA katika kuhamasisha watu kujitokeza na
kuchangia kampeni hii.
Mabalozi hawa wameiita
kampeni yao “Elimu Yao. Wajibu wetu” maana ya usemi huu ni kwa kila mtanzania ana
wajibu wa kuhakikisha mtoto wa kike anapewa haki yake ya kuwa na elimu bora. Haki
hii ya elimu inajumuisha mazingira mazuri ya kusomea. Hivyo huu ni wito kwa
watanzania, wafanyabiashara, wafanyakazi, wanawake watanzania waliofanikiwa na watanzania
wa ughaibuni kujitokeza kwa wingi na kuhusika moja kwa moja na jitihada hizi.
Changamoto ambazo mtoto wa
kike anakumbana nazo hususani anayetokea nyumbani kwenda shule ni pamoja na
kukosa muda wa kujisomea kutokana na kazi za nyumbani ambazo zinapelekea kuathiri
maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike, mimba na ndoa za utotoni ni kati ya
changamoto kubwa zinazowakumba wale waliopanga karibu na maeneo ya shule,
kutokana na hayo, Mabalozi hawa wameamua kujitolea kwa kuweka mpango mkakati
utakaosaidia ujenzi wa hosteli tano na kuendelea kati ya hizo 30 ambao TEA
imepanga kujenga.
Mpango mkakati huo ni pamoja
na kufanya kampeni katika vyomba mbalimbali vya habari nchini na kuandaa mbio za hisani ambapo hela zitakazopatikana
zitapelekwa katika mradi huo. Mabalozi hawa wanaamini kuwa tofali moja kutoka
kwa kila mtanzania linaweza kuleta mabadiliko “changia Tofali”. Unaweza kuchangia kwa kutuma neno "Changia
Tofali"kwenda namba 15564, na utakuwa umechangia Tshs 250/-. Changia mara
nyingi uwezavyo.
ERASMUS MTUI KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA YA MADEREVA
Meneja
Uendeshaji wa Kampuni ya Scania nchini Tanzania, Mark Cameron(kushoto)
akimkabidhi bendera ya Taifa dereva, ErasmusMtui ambaye ni mshindi wa mwaka
2011 anayekwenda kwenye mashindano ya Kimataifa ya Bingwa wa Mabingwa
yanayotarajiwa kufanyika Afrika
Kusini.Makabidhiano hayo yalifanyika makao makuu ya ofisi za Scania Dar es
Salaam
Erasmus Mtui akizungumza na waandishi wa habari
KAMPUNI ya Scania
Tanzania
leoimeandaahaflafupikumuagamshindiwamashindanoyamaderevayanayojulikanakama“Tanzania Driver Of The Year” yaliyofanyikakatikaviwanjavya
Biafra sikuyaJumamositarehe 19th November mwakajana.
Mr.
Erasmus
Mtui, mwenyeumriwamiaka 44
aliyebukamshindibaadayakufaulukatikangazizotetatuzashindanohilomwakajanaameajiriwakamaderevakatikakampuniyausafirishajiya
Super
Star Forwarders iliyokobarabarayaNyerere, Dar Es Salaam.
“Nimefanyamazoezinanimepatamafunzoyakutoshakabisa,
kwasasanikotayarikukabiliananashindanolijalo,
naahidikufanyajitihadazanguzoteiliniiwakilishevizurinchiyangu, benderaya Tanzania
ipeperukevizurikwenyemashindanohaya!” AlijigambaBw. Mtui.
Akiongeanawaandishiwahabari,
Bwana
Mark Cameron MenejaUendeshajiwakampuniyaScania Tanzania
alisemakwamba‘Derevandiokiungomuhimupekeekatikauchumi,
mazingiranausalama.
Maderevawenyeutaalamunawanaopendakaziyaohusaidiakuendeshakwausalamabarabarani,
hutumiamafutakidogo,
hiihusaidiakiwangokidogo cha
uchafuziwamazingira”.AlisemakwambaScaniailianzishamashindanoyamaderevakwamaraya
kwanza
mwaka 2003 katikanchizaulaya. Mashindanohayayalieneanakuwayadunianzima,
yakionyeshaumuhimuwautaalamukwamaderevapamojanakusisitizamafunzokwamaderevailikuboreshaufahamuwausalamabarabaraninauchafuziwamazingiraunaosababishwanamoshiwamagari.
Mr.
Cameron alimalizakwakusema
“Maderevandioutiwamgongowasektayausafirishaji.
Pamojanakutengenezamagarimakubwa bora,
salamanayanayotumiamafutavizuriScaniamudawoteinamuangaliamtualiyekonyumayausukani.
Kwamaraya
kwanza tumewezakufanikishamashindanohayahapa Tanzania,
tukonamshindiwetuMr.Mtuiambayeamejiandaavizuri,
tunamuamininatunatarajiaatatusababishiasifakubwa,
tunamtakiakila la kheri!.
Naye
Bi. Margaret Legga, afisamasokomsaidiziwakampuniyaScania Tanzania
alisemakwambamashindanohayayaliyopewajina la “BingwawaMabingwa”yatafanyikakatikamjiwa Sun City hukoAfrikayaKusinimapemamweziujaokuanziatarehe
09 hadi 11. Mashindanohayayatajumuishamaderevakutokamabaramenginekamabara la
Ulaya, Asia naAmerikayaKusini, kutokanchizaAfrikakunamaderevakutokanchiza
Botswana, Lesotho, Malawi, Namibia nasisi Tanzania.
WaandaajiwamashindanohayanikampuniyaSwiss organisation UICR Union Internationale Des
ChaffeursRoutiersna The South African RTMC Road Traffic Management Corporation,
Scanianimojawapoyawadhaminiwakuuwashindanohili.
Shindanohilihufanywamarambilikilamwaka.Mwakahuujumlayamadereva 105 kutokanchi
17 kotedunianiwatachuanakatikangazitofauti 6
zashindano.Mr.Mtuiatashindanakatikakitengo cha “Semi truck and trailor”
ambachoatapambanakikwelikwelikwanikiladerevaatatakiwakuonyeshaufundikwakuendeshanakupitavipimo
19 vyamchuano. Vipimohivinipamojanauendeshajiunaotumiamafutakidogo,
namnayakubebamzigokiusalama, kulifahamugarianaloendesha,
bilakusahauuendeshajimakinibarabarani. KufanyikakwashindanohilihapabaranikwetuAfrikakunatuongezeauwezekanowakufaulusisiwenyeji”
Alimaliza Bi.Legga.
Kama
mojawapoyawatengenezajiwamagarimakubwanamabasiwanaoongozaduniani,
Scaniainaendeleakuonyeshakujitoleakwakenakuwajibikakatikakujengasekta bora
yausafirishajiinayosababishafaidakwapandezote. Ili kufikiahili,
utaalamunauelewawamaderevanivitumuhimusana.
Mashindanoyamaderevayajulikanayokama“The Scania - Tanzanian Driver of the Year
competition”yanatoanafasikwamaderevakujadilinakuelezea mambo
ambayoyatasaidiakupunguzaajalibarabarani,
yataongezafaidabainayawadaumbalimbaliwasektahii.
Yanaonyeshapiakwawananchiwotevipajivyamaderevawetunamchangowaomuhimusanakwausalamawetuikiwanichangamotokwamaderevawenginekuongezaujuzi,
navijanakujiunganaajirahii.
Wateja wa Airtel sasa kutuma pesa Bure kupitia Airtel money
Kupata huduma ya Airtel money sasa piga *150*60# Bure
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa
kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure
Akiongea wakati wa
uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu
kirahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa
mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma na kuweza kuchagua
anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo,
kutoa pesa na mengine mengi
tumefanya hivi hii
ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na
kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja anauhuru wa
kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye
muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja
vilevile
tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo
kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na mteja
atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya
miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu
waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi
aliongeza” Mmbando
Airtel ni mtandao
ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye
mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini
kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za
kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma
za kibenki.
Kupitia Airtel
money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa,
kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na
huduma nyingine nyingi
Monday, July 30, 2012
BONDIA IBRAHIMU CLASS AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WA IDI PILI
Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com |
Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)