MKURUGENZI wa Global Publishers, Erick Shigongo
amewataka Wasanii kuacha tofauti zao katika kutetea maslahi ya nchi na si
vinginevyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana, na Mkurugenzi huyo alipokuwa
akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kuzulumiwa dola 3500 na msanii wa
Uganda Jose Chameleone.
Alisema ameshangazwa na baadhi ya Watanzania
kumchafua kwenye mitandao kwa kitendo chake cha kumdai msanii huyo wa Uganda,
fedha walizokubaliana katika mkataba ili kufanya onyesho la Tamasha la Usiku
wa Matumaini.
Shigongo alisema huu ni wakati kwa watanzania
kufahamu ukweli kuhusu hilo kutokana na ukweli kwamba msanii huyo, amekiuka
makubaliano ya mkataba wa kwanza ambao walikubaliana kufanya onyesho hilo
ghafla akageuka kudai fedha zaidi.
Alisema hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikubali
kuingia mkataba mwingine kwa mara ya pili kutokana na ukweli kwamba
alikwishafanya matangazo kuwa msanii huyo angekua mmoja wa wasanii ambao
wangefanya onyesho katika tamasha hilo.
“Kweli tulikubaliana mkataba mwingine nikamlipa
dola 8000 na kweli alikuja akafanya onyesho lakini baada ya hapo ndipo
nilipomdai fedha zangu dola 3500 alizochukua katika makubaliano ya
awali”alisema Shigongo.
Shigongo alisema si kweli kwamba alizuia
pasipoti ya msanii huyo wakati alipokuwa amepangisha chumba kwenye hoteli yake
bali kilichotokea ni msanii huyo kuondoka mwenyewe baada ya kudaiwa fedha hizo.
Katika hatua nyingine, Shigongo alisikitishwa
na kitendo cha msanii huyo akishirikiana na vijana wenzake kuvamia ubalozi wa
Tanzania nchini Uganda kwa madai ya kudai kurudishiwa pasipoti yake.
No comments :
Post a Comment