Mshambuliaji
wa Yanga, Said Bahanuz, akiwa amembeba mshambuliaji mwenzake, mfungaji
pekee wa bao la ushindi la Yanga dhidi ya APR, Hamis Kiiza,
wakishangilia baada ya mchezo huo wa hatua ya Nusu Fainali uliopigwa leo
jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kumalizika.
Katika
mchezo huo timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu huku timu hizo
zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana na hadi zilipomalizika
dakika 90 za mchezo huo timu hizo zilishindwa kufungana na kuingia
katika muda wa dakika za nyongeza.
Ilikuwa
ni dakika ya 10 katika dakika 15 za kwanza za kati ya 30 za muda wa
nyongeza, bao pekee a kichwa katika mchezo huo lililofungwa na Hamis
Kiiza limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo,
ambapo sasa timu hiyo itakipiga na Azam FC, siku ya Jumamosi katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza
alifunga bao hilo, baada ya krosi nzuri iliyopigwa na Haruna Niyonzima
baada ya mpira wa kurushwa 'chap chap' wakati Said Bahanuz akiwazuga
mabeki wa APR alipoanguka huku akiwalalamikia kumchezea vibaya huku
Niyonzima akianziwa mpira huo wa kurusha na kumimina korosi iliyomkuta
Kiiza na kuuzamisha mpira huo kimiani.
Dakika
tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita, alitolewa nje kwa
kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataukosa mchezo wa fainali kati
yao na Azam siku ya Jumamosi.
Wachezaji
wa Yanga, wakishangilia bao la Hamis Kiiza, lililodumu hadi mwisho wa
dakika za nyongeza kumalizika na kuwapa raha wana Yanga.
No comments :
Post a Comment