■Itatumia
mapambano yake kutangaza vivutio vya kitalii vya Tanzania
■
Kila bondia atakayegombea taji lake atavaa nembo zenye vivutio vya kitalii vya
Tanzania
Katika hali inayoashiria uzalendo
wa hali ya juu, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Mashariki ya
Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF) litaanza kuvitangaza vivutio vya kitalii vya
Tanzania katika mapambano yake yote ya ngumi ili viweze kujulikana zaidi
ulimwengumi.
Katika program yake ya “Utalii wa
Michezo” iliyowakilishwa na Rais wa shirikisho hilo katika bara la Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi, na kukubaliwa na mkutano
mkuu wa 29 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani
(IBF/USBA) uliomalizika hivi punde jijini Honolulu, Hawaii programu ya "Utalii
ya Michezo ya IBF" imegawanyika katika sehemu tatu:
1. Utalii wa Mikutano ya IBF
2.
Utalii
wa Kupanda Mlima Kilimanjaro kila mwaka (IBF Mount
Kilimanjaro Climb Expedition)
3. Utalii wa mapambano ya Ngumi
Ni katika “Utalii wa mapambano ya Ngumi” ambako shirikisho hili limeamua
kuvitangaza vivutio vya kitalii vya Tanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa taasisi
ya michezo hapa nchini na katika bara la Afrika kutumia mitandao yake kutangaza
vivutio vya kitalii vya nchi ya Afrika.
Akitangaza
nia ya IBF kuitangaza
Tanzania duniani kote Rais wa shirikisho hilo katika bara la Afrika,
Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi alisema kwamba ni
muhimu sisi Watanzania
tuliopewa nafasi katika taasisi za kimataifa tukatambua kuwa nchi yetu
inatakiwa kutangazwa.
Katika mkakati huu MTANZANIA Ngowi alisema
kuwa kwa sasa kuna mapambano kadhaa mbayo mabondia wa Kiafrika wanashiriki na
watayatumia kutangaza vivutio cya kitanzania. Alisema kuwa bondia Helen Joseph
wa Nigeria anayeishi Ghana atapambana na bondia Dahianna Santana wa nchi ya
Dominican Repubic na Helen ataitangaza Tanzania.
Mpambano huo utafanyika nchini
katika jiji la Santo Domingo nchini Dominican Republic, iliyoko katika eneo la Karibian karibu na Jamaica tarehe 12
August mwaka huu.
Aidha MTANZANIA Ramadhani Shauri
atapambana na bondia Sande Kizito wa Uganda katika mpambano uliopewa jina la “The Rumble in the City”
(Rurumai katika jiji) mpambano huo utafanyika siku ya Idd pili katika
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini dar-Es-Salaam.
Naye MTANZANIA Nasibu Ramadhani
atapimana ubavu na bondia Twalib Mubiru wa
Kenya kugombea mkanda wa IBF Afrika ya Mashariki na Kati katika uzito mwepesi
(lightweight) siku hiyo hiyo ya Idd pili, jijini dar-Es-Salaam.
Aidha, MTANZANIA Rajabu Maoja anayeishi katika jiji la
Tanga atapimana ubavu na bondia Gottlieb
Ndokosho bingwa wa ngumi nchini Namibia kugombea mkanda wa
IBF wa mabara katika uzito wa Unyoya. Mapambamo huo uliopewa jina la “The battle of the Kalahari Desert” (Vita
vya Jangwa la Kalahari) utafanyika katika jiji la Windhoek nchini Namibia.
Naye MTANZANIA Allen Kamote atapimana ubavu na bondia Wilson Masamba
wa Malawi katika mpambano wa kugombea mkanda wa IBF katika bara la
Afrika uzito mwepesi "Lightweight" jijini Arusha tarehe 27 Octoba mwaka
huu katika mpambano uliipewa jina la "TANZANITE Title" (Ubingwa wa Tanzanite). Mpambano
huo utafanyika katika jiji la Arusha na utaandaliwa na bondia wa zamani
wa taifa George Andrew chini ya kampuni yake ya
NIMEAMBATANISHA
PICHA YA ONESMO NGOWI AKIWAKILISHA UTALII WA MICHEZO, HAWAII, MAREKANI
Imetumwa
na;
Utawala
IBF katika bara la
Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi
No comments :
Post a Comment