TAMKO LA TASWA KUHUSU CECAFA
CHAMA
Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), kimesikitishwa na hatua ya
Baraza la Michezo la Vyama vya michezo la Afrika Mashariki (CECAFA),
kuwanyanyasa na kuwadhalilisha waandishi wa habari na wapiga picha
katika mchezo wa fainali Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa mjini
Dar es Salaam.
Kufuatia
kudhalilishwa huko kwa waandishi katika fainali hiyo ya michuano ya
kombe la Kagame kati ya Yanga na Azam, TASWA imelaani kitendo hicho na
kuwaondolea utu, udhalilishaji na unyanyasaji kulikosababishwa na baadhi
yao kutandikwa makofi na askari polisi mithiri ya vibaka.
Waandishi
wa habari za michezo wa Tanzania wamekuwa wasikivu, waadilifu na watu
wanaofuata taratibu, lakini katika fainali hiyo mara baada ya mchezo
walifanyiwa vitendo ambavyo havikulingana na tabia yao.
Lengo
la waandishi si kuleta vurugu bali kuhakikisha wananchi wanapata habari
kwa kila tukio lilikuwa linatokea uwanja, badala yake walionekana
hawana thamani mbele ya jamii inayowawakilisha.
TASWA
inalaani kitendo cha Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwa kutoa
agizo kwa polisi kuwazuia waandishi kuingia uwanjani kumalizia kazi zao
za kuhoji makocha na wachezaji, hali iliyosababisha vurugu.
CECAFA
walijenga urafiki wa karibu na waandishi kipindi chote cha mashindano
hayo na Kagame kwa lengo la kuyatangaza , lakini mwisho wa yote
walionekana kama taulo la deki limekuwa na thamini pale ambapo
linahitajika kwa deki, lakini baada ya hapo halina thamani tena.
Lakini
TASWA inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, kufuatia baadhi ya
waandishi kuonesha utovu wa nidhamu kama baadhi ya viongozi wa TFF na
CECAFA walivyodai kuwa walionesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kutoa
maneno ya kashfa na kutaka kumpiga Musonye
Kufuatia hatua hiyo TASWA imechukua maamuzi yafuatayo
1.Kutoandika jambo lolote linahusu Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki (CECAFA).
2.Kutoandika jambo lolote linahusu mashindano yoyote yaliyo chini ya CECAFA.
Ili
kuweza kufanya kazi pamoja na CECAFA,TASWA inataka kuombwa radhi na
CECAFA kutokana na kitendo hicho na kuwalipa fidia waandishi ambao
wamepoteza vifaa vya vya kazi na wengine kuhalibiwa vifaa vyao.
TASWA
inatoa onyo kali kwa baadhi ya vyama,viongozi na makampuni wenye tabia
ya kutotoa ushirikiano na dharau kwa waandishi wanapokuwa kwenye kazi
zao.
Juma Abbas Pinto
CHAIRMAN
Julai 30, 2012
Committee Members: A. Lucas, S. Jaba, G. Hoka, E.Kambili, O.Kapinga, Z. Chande
You might also like:
No comments :
Post a Comment