MWINGILIANO
wa masafa ya televisheni uliotokea hivi karibuni katika baadhi ya
maeneo ya Jiji la Mbeya umeelezwa kusababishwa na masafa yaliyokuwa
yakitumika kuchukuliwa na wamiliki wake halali walioyanunua.
Hayo
yamebainishwa leo na Meneja wa mamlaka ya mawazsiliano nchini(TCRA)
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Deogratius Moyo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake.
Moyo amesema kuwa masafa hayo hivi sasa yanatumika kutolea huduma za Interneti kwa makampuni yanayotoa huduma hiyo nchini.
Amesema
kwa watumiaji wa dishi ya Setilaiti wanatakiwa kufanya marekebisho ya
madishi yao ili waweze kupata masafa sahihi yanayorusha matangazo kwenye
masafa yaliyotengwa kwa ajili ya matangazo
ya Televisheni.
Akifafanua
zaidi, Meneja huyo amesema masafa ya sataelaiti katika C-Band huanzia
3.7GHZ hadi 4.2GHZ yametengwa kwa ajili ya intaneti barani Afrika huku
masafa hayo katika C- Band huanzia 3.4GHZ hadi 3.6GHZ ni kwa ajili ya
ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumzia
tatizo la masafa katika jiji la Mbeya, Moyo amesema kuwa kwa kuwa
wananchi wengi walifunga kifaa cha kunasa mawimbi (NLB) kwenye uelekeo
wa masafa ya intaneti ambayo wamiliki wake walikuwa hawajaanza
kuyatumia, na kuwa baada ya wamiliki halali kuyachukua imesabaisha
baadhi ya watu kukosa matangazo ya televisheni.
Meneja
huyo amesema masafa hayo kwa hivi sasa yanatumiwa na kampuni ya simu ya
Vodacom, hivyo watumiaji wengine hawana budi kuhama na kubadilisha
kifaa cha kunasa matangazo kwa njia ya sataelaiti (LNB).
Amesisitiza
wananchi kujiunga na mfumo wa digitali kwa kuwa ifikapo Desemba 31,
mwaka huu mitambo ya kurushia matangazo kwa njia ya analojia itazimwa
nchini huku akiusifia mfumo mpaya akisema ni salama, hauna madhara wala
gharama kubwa kwa mtumiaji.
Kwa hisani ya Joachim Nyambo
|
No comments :
Post a Comment