Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya MyWay
Entertainment, Paul Maganga (Kulia) akielezea juu ya tamasha maalum la siku ya
Wachaga lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika siku ya Jumamosi Julai
28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo pia litasindikizwa na bendi za
Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi vingine vya ngoma ya asili, (Kushoto) Ni
Fredrick Mtaki, Afisamahusiano wa kampuni hiyo.
BENDI zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga
Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la
siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
Akizungumza na waandishi wa habari
mapema leo ukumbi wa Udara habari Maelezo, ijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga walioandaa tamasha hilo
lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited,kupitia kinywaji cha Pepsi,
alisema siku hiyo
itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia
kujifunza mambo ya utamaduni wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine na
burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo, pamoja na vikundi vingine
vya ngoma ya asili ” alisema Maganga
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa
mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya
asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari,
ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku
hiyo.
Aidha, Siboka alisema baada ya
Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa
wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
Aidha, Maganga alisema kua,
wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini
ilikuwezesha jamii kutambua mila zao sambamba na kudumisha utamaduni wa
Mtanzania kwa kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha
mahusiano baina ya makabila mbalimbali nchini Tanzania.
Pia anasema kua, watazania watakao
hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa tamaduni zao
yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii
zao.
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa
tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro, SBC
Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou
Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili
Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel
&Tours, Dotnata Decorations.
No comments :
Post a Comment