Wachezaji wa Azam wakishangilia bao lililofungwa na John Bocco.
TIMU
ya Azam Fc, leo imetinga hatua ya Fainali na kumsubiri mshindi kati ya
Yanga ya Dar es Salaam ama APR ya Rwanda, baada ya kuichapa AS Vita kwa
mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa leo mchana mida ya saa nane katika
Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Hadi
mapumziko, AS Vita walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na
Mfongang Alfred, katika dakika ya 34, baada ya kuunasa mpira uliopigwa
na Ibrahim Shikanda na kuichambua ngome ya Azam kabla ya kuachia shuti
kali lililomshinda kipa wa Azam, Deo Munishi ‘Dida’.
Vita
walipata pigo dakika ya 41, baada ya mchezaji wao, Issama Mpeko,
kutolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Azam ilisawazisha bao
hilo, kupitia kwa John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 68 aliyeunganisha kwa
kichwa krosi ya Kipre Tchetche, kutoka wingi ya kulia.
Mrisho
Khalfan Ngassa aliyeingia kutokea benchi kipindi cha pili aliifungia
Azam bao la ushindi dakika ya 89, akimalizia pasi ya Salum Abubakar
‘Sure Boy’. Baada ya kufunga bao hilo, Mrisho alikwenda moja kwa moja
kwa mashabiki wa Yanga na kushangilia nao, badala ya mashabiki wa Azam.
No comments :
Post a Comment