Diwani
wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye
trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel
Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta manne, kwenye
Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT,
Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao
kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana
kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja ambayo
inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu
ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki katika kipindi cha miaka minne
kwa udhamini wa diwani huyo.
Diwani
wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati, akimkabidhi funguo za trekta,
mkulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani, katika hafla ya diwani huyo
kukabidhi matrekta manne wakulima kutoka kata hiyo, kwenye Ofisi za
Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge
jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao
kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana
kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja ambayo
inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu
ya bei hiyo na kisha kulipa zilizobaki katika kipindi cha miaka minne
kwa udhamini wa diwani huyo. Wengine, ni wakulima wa kata hiyo ya
Kwadelo, Alifa Hurufya, Gabriel Galahenga (wapili kushoto) na Meneja wa
Mradi wa SUMA JKT, Kanali Felix Samillan.
No comments :
Post a Comment